Na,
Francisca Swai- Mahakama, Musoma
Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Musoma wameaaswa kuchukua tahadhari wanapotoa
huduma kwa wananchi ili
kuepukana na virusi vya Corona vinavyosababishwa ugonjwa wa COVID-19, ukiwemo ugonjwa wa Homa ya Ini (HEPATITIS B).
Tahadhari hiyo ilitolewa hivi karibuni
na Mwenyekiti wa Kamati ya COVID – 19, Elimu ya Afya kwa Jamii Mkoa wa Mara,
Dkt. Theophil Kayombo alipokuwa akitoa elimu juu ya hatari ya magonjwa mawili yanayosababishwa na virusi ambayo ni ugonjwa wa COVID-19 na Homa ya Ini.
‘‘Vema katika kipindi hiki kuchukua
tahadhari ya hali ya juu wakati wa kutoa huduma kwa wananchi. Daktari huyo
alisema, huwezi kujua unamhudumia mteja aliye
katika hali gani ya kiafya,’’alisema Dkt. Kayombo.
Aliongeza kwamba ingawa dalili zote zinaeleweka za ugonjwa wa
COVID-19 ambazo ni kuwa homa kali, mafua makali, kuumwa na koo pamoja
na kikohozi kikali lakini bado sio watu wote wanaonyesha dalili hizo kwa
haraka.
‘Tunachotakiwa kufanya ni kuzingatia
maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa (mask) na kunawa mikono mara kwa mara.’’alisisitiza.
Daktari huyo aliwaasa watumishi pamoja na jamii kwa ujumla kuepuka mikusanyiko isiyoyalazima, kuepuka kukaa sehemu zenye mikusanyiko kwa muda mrefu kama vile sokoni na kuzingatia mashart yanaelekezwa na Serikali, ili kujilinda wenyewe, familia zetu na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa HEPATITIS B , Dkt. Kayombo alisema ini lina kazi nyingi
mwili na moja wapo ya kazi kubwa
ni kuchuja sumu mwilini, Hivyo
inapotokea kiungo hicho kushindwa kufanya kazi hiyo inamaana mwili wako uko
katika hatari kubwa.
Dkt, Kayombo alisema ugonjwa huo unasambaa kwa kupitia
majimaji yanayotoka katika mwili pamoja na damu. Na Takwimu za Shirika la Afya
Duniani (WHO) zinaonyesha takriban watu 600, 000 hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.
Kwa
upande wake, Mtendaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Musoma Bw, Festo Chonya alimshukuru muwezeshaji huyo kwa kutoa
elimu hiyo muhimu kwa watumishi na huku akiwapamoyo katika kutekeleza majukumu
yao ya kila siku.
Aliahidi kuweka utaratibu wa watumishi wote waweze kupima ugonjwa wa homa ya Ini
kwa kuwa mtumishi anapokuwa na afya bora basi na mwajiri anakuwa na uhakika wa
kupata matokeo mazuri katika kazi zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni