Alhamisi, 16 Aprili 2020

VIONGOZI WA MAHAKAMA BUKOBA NA WADAU WAJADILI KUPUNGUZA MSONGAMANO

Jaji Mfawidhi wa  Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba , Mhe. Lucia Kairo (katikati)akisisitiza  jambo  leo kuhusu  ufunguaji wa mashauri kwa njia ya mtandao kwa wadau wa Mahakama ili kupunguza msongamano katika maeneo ya Mahakama na magerezani kwa upande wa mahabusu na wafungwa ili kuepuka maambukizi ya  ugonjwa wa Corona .

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe.   Dkt. Ntemi Kilekamajenga  (wa pili kutoka kulia)  akisisitiza namna bora  ya kutumia adhabu mbadala badala ya vifungo magerezani kwa baadhi ya makosa ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa mahabusu/wafungwa magerezani wakati wa  kipindi cha ugonjwa wa Corona  kwa Wahe. Mahakimu.
Baadhi ya Watumishi wa  Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba  na wadau wa Mahakama wakimsikiliza , Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba,  Mhe.Lucia  Kairo (hayupo pichani) katika kikao maalumu na wadau wa Mahakama kuangalia namna bora ya kupunguza msongamano katika maeneo ya Mahakama na  magerezani kwa upande  wa mahabusu na wafungwa.

Baadhi ya Watumishi wa  Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba  na wadau wa Mahakama wakimsikiliza , Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba,  Mhe.Lucia  Kairo (hayupo pichani) katika kikao maalumu na wadau wa Mahakama kuangalia namna bora ya kupunguza msongamano katika maeneo ya Mahakama, yakiwemo  maeneo ya magerezani kwa upande  wa mahabusu na wafungwa.

(Picha  na Ahmed Mbilinyi – Mahakama Kuu Kanda, Bukoba)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni