Jumatatu, 4 Mei 2020

HAKIMU MKAZI MFAWIDHI MAHAKAMA YA WILAYA YA GEITA AFARIKI DUNIA

     

  TANZIA  

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Geita Mhe. Gabriel Nimrod Kurwijila kilichotokea jana jioni tarehe 3/5/2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taratibu na mipango ya mazishi inafanywa na Mahakama kwa kushirikiana na familia yake. Taratibu za mazishi zitajulikana baadaye.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE


                         



                             





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni