Na Innocent Kansha- Mahakama
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es
salaam jana ilitoa hukumu tatu za mashauri ya mauaji kwa njia
ya Mahakama Mtandao maarufu kama “Video Conference” kwa kushirikiana na
Magereza ya Keko na Segerea Jijini Dar es salaam, huku ikiahirisha mashauri
mawili.
Mashauri matano ya mauaji yalisikilizwa
mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, Mhe.
Lameck Mlacha kwa kutumika njia hiyo.
Kati ya mashauri hayo matatu yalisikilizwa
na kutolewa hukumu, kwa washitakiwa Hassan
Kidingiri na Mickidadi Matunguru, Mhe. aliwatia hatiani kwa kosa
la mauaji chini ya kifungu 195 cha kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Aidha, kila mshitakiwa alihukumiwa
kwenda jela miaka minne, akieleza chanzo cha kosa la mauaji hayo mahakamani
hapo Wakili wa Serikali Mwandamizi Adolph Kisima, alidai kuwa ni ugomvi
ulitokana na kugombea pombe aina ya kiroba na kupelekea mshitakiwa Kidigiri
kumchoma kisu kifuani marehemu Isaya Mwakifuna.
Wakili Adoph aliieleza mahakama kuwa katika tukio la pili
la mauaji mshitakiwa Batunguru alifika
nyumbani kwa marehemu Salehe Nassoro usiku akiwa amelewa na kuanzisha ugomvi na
kumpiga sehemu ya kichwa na kusababisha mauti.
Katika kosa lingine la mauaji Jaji Mfawidhi huyo, alimtia hatini mshitakiwa Fred Devid na
kuhukumu adhabu ya kifungo cha nje chenye masharti ya kutotenda kosa lolote
ndani ya miezi 12, na endapo atafanya kosa lolote ndani ya muda huo basi
ataletwa mahakamani kwa ajili ya kupewa adhabu nyingine.
Akielezea mahakamani hapo Wakili wa
Serikali Mwandamizi Mkunde Mshanga alidai mshitakiwa Devid akiwa kwenye eneo lake la ulinzi maeneo
ya Mbagala Kuu wakati wa usiku alitokea marehemu akiwa anagombana na mtu
aliyejulikana kwa jina moja Irene kwa kutumia mawe ndipo mshitakiwa akiwa anajihami
alichomoa kisu na mchoma marehemu Muddy Mkoye.
Mashauri mengine ya mauaji mawili
yaliyoko kwenye hukumu yaliahirishwa mahakamani hapo kwa sababu
ambazo hazikuweza kuzuilika na yamepangwa kutolewa hukumu Mei 19, mwaka
huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni