Na Lydia Churi- Mahakama
Watumishi wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Divisheni ya Biashara Dar es salaam wameanzisha utaratibu wa kuwa
na sala ya pamoja kwa muda wa dakika 5 kila siku asubuhi kabla ya kuanza kutekeleza
majukumu yao.
Akizungumza wakati wa mahojiano
na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania, Mtendaji wa
Divisheni ya Biashara Bw. Benjamin Mlimbila alisema madhumuni ya kuanzisha utaratibu huo wa watumishi
wote kukutana kila siku asubuhi ni kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumwomba kuwawezesha kutekeleza wajibu wao pamoja na kuiombea Mahakama ya Tanzania kwa ujumla.
“Pamoja na kushukuru na
kumwomba Mungu kutuwezesha kutekeleza wajibu wetu kwa haki, pia tumeamua
kutumia nafasi hii kuliombea taifa letu dhidi ya ugonjwa wa COVID 19
unaosababishwa na virusi vya Corona”, alisema Mtendaji huyo.
Akielezea utaratibu wa
kufanyika kwa sala hiyo, Bw. Mlimbila alisema imekuwa ikifanyika kwa kuhusisha
dini zote.
Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara wakiwa kwenye kipindi cha sala ya asubuhi kabla ya kuanza kazi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Mhe. Patricia Fikirini akiwa kwenye kipindi cha sala ya asubuhi kabla ya kuanza kazi.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Bw. Benjamin Mlimbila akizungumza wakati akiongoza sala ya Asubuhi.
Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara wakiwa kwenye kipindi cha sala ya asubuhi kabla ya kuanza kazi.
Mtumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara akiongoza sala kwa upande wa Dini ya Kiislamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni