Na. Francisca Swai- Mahakama Kuu Musoma
Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Musoma, imesikiliza jumla ya mashauri kumi 18 kwa njia ya
Mahakama Mtandao ‘Video Conference’ tangu ilipoanza kutumia teknolojia hiyo
Mei 5, mwaka huu.
Akizungumzia
matumizi ya Mahakama Mtandao, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda
ya Musoma Mhe, John Kahyoza alisema walianza kusikiliza mashauri mawili yote
yakiwa yanayohusu maombi ya kukata rufaa nje ya muda yalisikilizwa mbele yake
wakati wafungwa wakiwa katika gereza la Musoma bila ya wao kufika Mahakamani.
Jaji Kahyoza
alifafanua kuwa mashauri 10 yalisikilizwa
mbele yake, manne yalisikilizwa na
Mhe, Jaji, Zephrine Galeba na mashauri
yaliyobakia yalisikilizwa na Mhe, Jaji Ephery Kisanya.
‘‘Mahakama ya
Tanzania ilianza kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao muda mrefu katika
baadhi ya Mahakama nchini ikiwa ni katika kutekeleza mpango mkakati wake wa
miaka mitano (2015/2016 – 2019/2020). Hata hivyo jitihada hizo zimetiliwa
mkazo kama njia ya kuepuka kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona
vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID 19)”, alisema Jaji Kahyoza.
Aliongeza kwamba
Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma pia imeanza kusikiliza mashauri kwa njia hiyo
Mei 12, mwaka huu, ambapo mashauri matatu yalisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Mhe, Rahim Mushi na kuaihirishwa bila ya Wakili wa Serikali Mhe, Jesse
Temba na washtakiwa kufika mahakamani hapo.
Jaji Kahyoza
alisisitiza kwamba Mahakama hiyo, itaendelea kusikiliza mashauri kwa mtandao.
Pia itawekeana ratiba maalumu na Mahakama ya Hakimu Mkazi, zikiwemo za Wilaya
ili kutekeleza maagizo ya viongozi wa juu wa Mahakama wakiwemo viongozi wa
kitaifa wanaosisistiza kuepuka msongamano na mikusanyiko hasa katika kipindi
hiki cha janga la Corona.
|
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe, John Kahyoza akizungumzia matumizi ya Mahakama Mtandao ofisini kwake jana.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe, Zephrine Galeba ya akiendesha shauri kwa njia ya Mahakama Mtandao katika ukumbi wa Mahakama hiyo jana.
|
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Mhe.Rahim Mushi akisikiliza
shauri kwa njia hiyo.
(Picha
na Francisca Swai –Mahakama Kuu Musoma).
|
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni