Jumanne, 12 Mei 2020

MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA


                                                          TANZIA

Marehemu Mwanaisha Rashid Manase.

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake, Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mwanaisha Rashid Manase kilichotokea jana asubuhi tarehe 11/5/2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taratibu na mipango ya mazishi inafanywa na Mahakama kwa kushirikiana na familia yake. Marehemu atasafirishwa kesho tarehe 13/05/2020 saa 10.00 jioni kuelekea Same, mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.

Marehemu alizaliwa tarehe 18/06/1962 na aliajiriwa tarehe 5/04/1981 Mahakama ya Mwanzo Same.

Katika utumishi wake marehemu, pia alifanya kazi,Mahakama za Wilaya Kilwa, Shinyanga, Temeke na Ilala, Mahakama ya Mwanzo Shinyanga, Mbagala Buguruni na Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.


BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni