Na Magreth Kinabo na Innocent
Kansha- Mahakama, Chato
Mahakama ya Wilaya ya Chato imetoa hukumu zaidi ya 18 zinazotokana na makosa ya
ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika kipindi cha miezi minne baada
ya jamii kuwa na uelewa juu ya suala hilo na kuweka mikakati ya kutatua
changamoto hiyo.
Akizungumza na Maofisa Habari wa Mahakama ya Tanzania, Juni 9, mwaka huu
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Odira Amworo amesema mashauri yanayoongoza kusikilizwa mahakamani
hapo ni ya vitendo vya ukatili wa kijinsia huku akitolea mfano ubakaji na mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi.
Alisema Mahakama hiyo, imekuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto
hiyo, ambapo imeshatoa maamuzi mbalimbali.
‘‘Ongezeko la mashauri haya mahakamani hapa limetokana na mwamko wa jamii
kuwa na uelewa wa masuala ya ukatili na
unyanyasaji wa kijinsia baada ya kutolewa kwa elimu juu ya masuala
haya, ambayo tuliitoa mashuleni wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria, ambapo
tuliwaelimisha watoto wa kike wanapofanyiwa vitendo hivyo watoe taarifa kwa
wazazi na kituo cha polisi,’’ alisema
Mhe. Amworo.
Akifafanua juu ya adhabu zilizolewa kwenye hukumu hizo, Mhe Amworo alisema kwamba imetoa adhabu ya kifungo cha maisha
jela katika mashauri matatu, na miaka 30 jela mashauri mengine ili kutoa fundisho kwa watu wengine.
Aliwataka watoto wa kike kutokubali kurubuniwa kushiriki katika vitendo vya ngono, bali wakijite katika masomo. Alisema takwimu hizo ni za tangu baada ya uzinduzi uliofanyika mwaka jana hadi Juni mwaka huu.
Aliwataka watoto wa kike kutokubali kurubuniwa kushiriki katika vitendo vya ngono, bali wakijite katika masomo. Alisema takwimu hizo ni za tangu baada ya uzinduzi uliofanyika mwaka jana hadi Juni mwaka huu.
Hakimu huyo alifafanua kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokana na kuvunjika kwa
baadhi ya ndoa, hivyo Mama anapobaki na mtoto wa kike chini ya umri wa miaka 10
baba wa kambo huweza kuwafanyia watoto vitendo hivyo.
Aliyataja mashauri mengine yanayosikilizwa na Mahakama hiyo kuwa ni makosa
ya uvuvi haramu, kuvamia hifadhi za taifa kinyume cha sheria na kukutwa na dawa
za kulevya.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Chato, alisema umesaidia kutatua tatizo la utunzaji wa nyaraka kiholela ,kuwa sasa
linafanywa kwa ufanisi na hakuna tena malalamiko ya upotevu wa nyaraka,
ukilinganisha na lile jengo la zamani la Mahakama ya Mwanzo Chato Mjini ambalo mara kwa mara kulikuwa na
upotevu wa nyaraka mbalimbali.
‘‘Hivi sasa tuna jengo maalumu la utunzaji nyaraka mbalimbali, ambapo zinatunzwa
vizuri na kwa utaratibu uliopangwa,’’
alisititiza.
Kuhusu hali ya usikilizwaji wa mashauri, alisema kulikuwa na mashauri ya mlundikano 50, kutokana na upungufu wa Mahakimu, lakini
sasa yamebaki mashauri matano baada ya
kuongezeka Mahakimu sita. Awali kulikuwa na Mahakimu watatu tu. Hatua hiyo itasaidia mashauri kumalizika ndani ya mwezi au wiki tatu isipokuwa makosa
ya mauaji, kubaka, na kosa la kumpatia ujauzito mwanafunzi ambayo upelelezi wake
huchukua muda mrefu.
Kwa upande wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
wamefanikiwa kuhuisha mashauri katika Mfumo wa Kuratibu na Kusajili Mashauri
kwa njia ya Kielektroniki (JSDS 11) tangu
mwaka 2013 hadi sasa mashari 1, 348 ya madai na jinai. Kati ya mashauri hayo
169 ni hai.
Pia mashauri yaliyofunguliwa kuanzia
mwezi Januari hadi sasa ni 234, yaliyotolewa maamuzi ni
mashauri 259. Mashauri yaliyofunguliwa kwa njia ya mtandao ni sita, lakini
mawili yalikataliwa.
Tunamtumia mlinzi na mhudumu wa ofisi kuhuisha takwimu kwa njia TEHAMA baada
ya kuwapatia mafunzo na kufungua mashauri kwa njia ya mtandao.
Alitoa wito kwa jamii kutotumia nguvu ya Umma kutafuta haki zao na kujichukulia
sheria mkononi badala yake waitumie miundombinu ya kisasa ya Mahakama hiyo ili
kuwezesha migogoro yao kutatuliwa wakati, weledi na haki.
Naye Mlinzi wa Mahakama hiyo, Tabitha Andrew alisema anaifanya kazi hiyo
baada ya kupatiwa mafunzo ya siku moja kutoka kwa wataalamu wa TEHAMA kutoka Makao Makuu.
‘‘Nimefanikiwa kuifanya kazi hii kwa kuwa ninapata ushirikino wa kutosha
kutoka kwa watumishi wenzangu. Nina matarajio
ya kujifunza zaidi katika eneo hili ili niweze kufikia kiwango cha juu na
kuisaidia taifa la Tanzania,’’ alisema
Andrew ambaye ni mwajiriwa mpya kuanzia Novemba Mosi mwaka huu.
Kwa upande wake Afisa Tawala wa Mahakama
ya Wilaya ya Chato, Bw. Faulent
Kiowi alielezea kwamba baada ya kuanza kufanya kazi kwenye jengo
jipya wamefanikiwa kujenga imani kwa wananchi na ifikapo muda wa saa 7.00 mchana wanakuwa wameshahudumiwa
ili waweze kuendelea shughuli nyingine. Pia tatizo la kuhairisha mashauri
mara kwa mara halipo kwa sababu kila mtumishi ana chumba chake cha kufanyiakazi na vitendea
kazi.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Chato Bw. Masumbuko Sobilwe, alisema awali wakazi wa wilaya hiyo walikuwa
wakipata huduma za kimahakama kwenye Wilaya ya Biharamulo, ambapo umbali wake
ni zaidi ya kilomita 70.
‘‘Hivi sasa wananchi wanafurahia kupatiwa huduma za Mahakama karibu na haki
inatolewa kwa wakati. Pia kiwango cha malalamiko kimepungua, kwa kuwa zamani
walikuwa wanalalamikia kutozwa tozo za kuwapeleka ndugu za mahakamani, lakini
suala hili sasa halipo,’’ alisema Sobilwe. Huku akishukuru Serikali kwa
kuwapatia huduma hiyo karibu.
Mahakama hiyo kwa mwaka hupokea wastani wa mashauri 400 na inahudumia watu 1,600 kwa mwaka.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Chato, Mhe. Odira Amworo akizungumzia kuhusu uboreshajji wa miundombinu ulivyorahisha utoaji wa haki kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni