Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi
akiongoza kikao cha Baraza la Elimu ya Sheria la Tanzania Bara, kwa njia ya
Mkutano Mtandao leo Jijini Dar es Salaam
huku baadhi ya wajumbe wawili wakishiriki kwa mtandao nje ya jiji hilo. Jaji Kiongozi ambaye ni Mwenyekiti
wa baraza hilo, ameongoza kikao hicho
cha tathmini ya mchakato wa kupokea maombi , usaili wa kuwapokea na kuwakubali
mawakili wapya uliofanyika hivi karibuni.
Katibu wa
Baraza la Elimu ya Sheria la Tanzania Bara, ambaye pia Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Messe Chaba akitoa tathimini kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa
kikao hicho, Dkt. Erasmo Nyika ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School )akichangia hoja.
|
Mjumbe wa
kikao hicho, Aisha Sinda ambaye ni mjumbe wa Baraza na ni Wakili wa kujitegemea akichangia hoja.
|
(Picha na
Innocent Kansha- Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni