Jumatano, 8 Julai 2020

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA ATEMBELEA MAHAKAMA KUU KANDA YA KIGOMA

Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe.  Amon Mpanju(kulia)  leo ametembelea Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma ili kujionea hali ya utoaji  huduma ya haki  kwa wananchi hususan wanyonge, ikiwemo ya Msaada wa Kisheria kabla ya uzinduzi wa  Kamati ya Uratibu  wa Huduma  ya Msaada  wa Kisheria  Mkoa  wa Kigoma.  

Aidha Mpanju amefanya  mazungumzo na  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma, Mhe. Ilvin Mugeta ambaye alimwelezea ubora  wa huduma inayotolewa katika Mahakama hiyo kupitia Mahakama Mtandao  na kuhusu kutoa ofisi  kutoka jengo hilo kwa ajili ya  huduma ya msaada wa kisheria.



Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe.  Amon Mpanju (wa tatu kulia)  akiwa katika picha ya pamoja kwenye jengo jipya la  Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma. Wa pili kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma, Mhe. Ilvin Mugeta.


(Picha na Festor Sanga- Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni