Na Magreth Kinabo na Innocent Kansha
- Mahakama
Jumla ya mashauri ya jinai 24,698 yalifunguliwa katika
ngazi mbalimbali za Mahakama nchini na kati ya hayo, mashauri 25,950, sawa na asilimia 105.06 ya mashauri yote yaliyofunguliwa yalisikilizwa na kumalizika kati ya mwezi Januari na Julai Mosi, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith Kamugisha alisema mashauri hayo yalifunguliwa katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuanzia Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu pamoja na Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya nchini kati ya mwezi Januari na Julai Mosi mwaka huu .
Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith Kamugisha alisema mashauri hayo yalifunguliwa katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuanzia Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu pamoja na Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya nchini kati ya mwezi Januari na Julai Mosi mwaka huu .
Akitoa taarifa ya uendeshaji wa mashauri hayo kwenye
kikao kazi cha robo mwaka ya pili ya
mwaka wa kimahakama cha mwaka huu
kilichohusisha wadau wa Kamati ya Kitaifa ya Haki Jinai alisema Mahakama hivi sasa ina uwezo wa
kusikiliza mashauri yote yanayoingia mahakamani ili kuhakikisha haki
inapatikana kwa wakati.
‘‘Taarifa hii inaelezea hali ya
ufunguaji na usikilizaji wa mashauri ya jinai kwa kipindi cha Januari hadi
Julai Mosi, 2020 kwa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi
na Mahakama za Wilaya nchi nzima.“Kwa
upande wa Mahakama ya Rufani Tanzania, jumla ya mashauri ya jinai 297 yalifunguliwa na mashauri 210 yalisikilizwa sawa na asilimia 70.7 ya mashauri yote yaliyofunguliwa
katika kipindi hicho,’’ alisema Kamugisha huku akisema wastani wa mzigo wa mashauri ni 737 kwa jopo la majaji
wa tatu.
Alisema Mahakama Kuu ya Tanzania, mashauri ya jinai
2,561 yalifunguliwa na 2,618 yalisikilizwa sawa na asilimia 102.2. Wastani wa
mzigo wa mashauri ni 345 kwa kila Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kamugisha alisema katika Mahakama za Hakimu Mkazi jumla ya mashauri 5,338
yalifunguliwa, 5,566 yalisikilizwa sawa na asilimia 104.3 ya mashauri
ya jinai yaliyofunguliwa. Hivyo wastani wa mzigo wa mashauri ni 198
kwa kila Hakimu.
“Mahakama za Wilaya
mashauri 16,169 yalifunguliwa, mashauri 17,254 yalisikilizwa sawa na asilimia
97.5.Hadi kufikia Julai Mosi, 2020 wastani wa mzigo wa mashauri kwa Mahakama za
Wilaya ni 96 kwa kila Hakimu,”alisisitiza
.
Aliongeza
kwamba mashauri 333 yalifungiliwa katika
Mahakama za Watoto, 302 yalisikilizwa sawa na asilimia 90.6.
Kwa upande wa ofisi
ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, ambayo imewakilishwa na Naibu
Kamishna wa Polisi Bw.Saleh Ambika alieleza kuwa lengo kuu la ofisi yake ni
kuhakikisha upelelezi wa makosa ya jinai unafanyika na unakamilika kwa haraka
zaidi kadri iwezekanavyo.
“Upelelezi wa makosa
ya jinai una hatua mbalimbali na unahusisha taasisi mbalimbali za mfumo wa haki
jinai kuna wakati mwingine Polisi wanahitaji kupata ripoti zinazotoka mamlaka
nyingine kukamilisha upelelezi ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kwa wakati,”
alisema Ambika.
Alifafanua kuwa upelelezi
unaohusisha sampuli za kitu fulani, Kitengo cha Upelelezi lazima kishirikiane na
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakatiKmwingine sio rahisi kupata ripoti kwa
kadri ya matarajio ya upelelezi wako, pia taasisi hiyo inataratibu zake za
kiuchunguzi ili kukamilisha hilo,
Ambike alisema ushirikiano
wadau hao upo kwa kiwango cha kutosha, hivyo hilo ndio lengo la kamati hiyo ni kuisaidia Mahakama ya Tanzania kufikia ajenda ya kupunguza mlundikano wa
mashauri mahakamani.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Huduma za Uangalizi kwa
wafungwa wanaotumikia vifungo vya nje ya Magereza, Bw. Charles Nganze alisema
wafungwa 706 walitumikia adhabu mbadala ya kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo ya Makaburi ya Kinondoni, mabwawa ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) , wizara na zahanati mbalimbali.
Naye Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Bw,Willington Kamuhuza, alishukuru jitihada
zilizofanywa na wadau hao zimesaidia kupunguza msongamano wafungwa kwa
asilimia 0.73.Pia aliongeza kwamba kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) jumla ya mikoa 16 iliyo na magereza mashauri hayo yamesikilizwa kwa
njia ya Mahakama Mtandao baada ya kuwezeshwa kuwa na vifaa vya TEHAMA kutoka
Mahakama ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kitaifa ya Uondoshaji wa Mashauri ya Jinai, ambaye pia ni
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah
Sarwatt alisema lengo kikao hicho ni kutathmini utendaji kazi na kupanga mikakati ya kupunguza mlundikano wa mashauri ya aina hiyo.
Mwakilishi kutoka katika ofisi ya Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), ambayo
imewakilishwa na Naibu Kamishna wa Polisi. Bw.Saleh Ambika akifafanua jambo.
|
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Bw,Willington Kamuhuza,(kushoto)
akizungumza jambo kwenye kikao hicho. (Kulia ) ni Mkurugenzi wa
Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith
Kamugisha.
Baadhi ya wadau hao wakiwa katika kikao hicho.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni