Mahakama Kuu Tanzania Kanda
ya Kigoma,
imefanikiwa kusikiliza mashauri kwa asilimia 77 baada ya
kujiwekea malengo ili hakikisha haki
inatolewa kwa wakati tofauti na Mkakati wa
Mahakama ya Tanzania.
Akizungumzia
kuhusu suala hilo, Jaji Mfawidhi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma Mhe. Ilvin Mugeta alisema kanda hiyo ina mpango iliyojiwekea wa muda wa usikilizaji wa
mashauri.
‘‘Mpango huu unalenga kusimamia utoaji haki
kwa haraka katika viwango vya kanda tulivyojiwekea ambapo Mahakama za Mwanzo
kesi itadumu kwa (miezi mitatu), Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi zitadumu
(miezi minne) na Mahakama Kuu (miezi
sita), akitolea mfano kwa upande wa Mahakama Kuu kuanzia Januari hadi Juni
mwaka huu walipokea mashauri 190 na yaliyomalizika ni mashauri 165 sawa na
asilimia 77,’’ alisema Jaji Mugeta.
Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa Miaka Mitano
(2015/16 hadi 2019/20), inasisitiza utoaji haki kwa wote na kwa wakati ambapo
imejiwekea muda wa kumalizika kwa shauri mahakamani. Katika Mahakama za Hakimu
Mkazi pamoja na Mahakama za wilaya shauri linatakiwa kumalizika ndani ya
miezi 12, Mahakama Kuu ndani ya miaka miwili na Mahakama za Mwanzo ni miezi sita.
Jaji Mugeta aliongeza kwamba alifanya ziara katika Wilaya
za Kasulu na Kibondo Juni 23
hadi 24 mwaka huu, ambapo alikabidhi kwa Wakuu wa Magereza
ya Kasulu na Kibondo vifaa vya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ili kuwezesha
usikilizaji wa mashauri kwa njia ya Mahakama
Mtandao ‘Video Conference’.
Alivitaja vifaa vilivyokabidhiwa kwenye magereza hayo kuwa ni Televisheni (TV
inch 32), kompyuta mpakato (Laptop), Modem zenye laini za simu zenye kifurushi cha GB 34
kwa kila Gereza .
‘‘Vifaa hivyo vya TEHAMA vitapunguza adha ya mahabusu
na wafungwa kukosa kufika Mahakamani kutokana na changamoto ya usafiri,’’
alisema Mhe. Mugeta.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo ni utekelezaji kwa vitendo wa maagizo ya Jaji
Mkuu wa Tanzania, kuhusu kuongeza kasi
ya matumizi ya TEHAMA katika kusajili na
kusikiliza mashauri kwa mtandao.
Aidha, Jaji Mugeta
alisema usambazaji wa vifaa hivyo
ni utekelezaji dhahiri wa mpango wa ndani wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Kigoma uliozinduliwa rasmi
katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria iliyofanyika Februari 6, mwaka huu.
Pamoja
na kukabidhi vifaa hivyo, Jaji Mugeta
alitembelea pia ofisi za wakuu wa Wilaya za Uvinza, Kakonko, Kibondo, Kasulu na Buhigwe kwa lengo la kuhimiza kamati za
maadili za Mahakimu na Maafisa wa mahakama kukutana kwa mujibu wa Muongozo wa
Uendendeshaji wa Kamati za Maadili.
Jaji Mugeta katika ziara hiyo aliambatana na Naibu
Msajili na Mtendaji wa Mahakama hiyo ambapo walitembelea viwanja vya Mahakama
ambavyo vina vinatarajiwa kujengwa Mahakama
za Wilaya za Uvinza, Buhigwe na Kakonko.
Picha ya pamoja ya viongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma na uongozi wa gereza la Kibondo.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni