Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania Mhe. Eliezer Feleshi amewataka Mahakimu wa Mahakama za Hakimu
Mkazi na Mahakama za wilaya kutoa kipaumbele kwenye mashauri yanayohusu Mirathi,
Ndoa, na Kuasili mtoto.
Jaji Kiongozi ameyasema
hayo jana alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mahakimu wa Mahakama za Hakimu
Mkazi na Mahakama za wilaya waliopangiwa vituo vya kazi baada ya kumaliza Mpango
Maalumu wa kufanya kazi kwenye Mahakama za Mwanzo na wilaya. Mahakimu hao ni
wale waliokuwa wasaidizi wa kisheria wa Majaji ambao hivi karibuni waliapishwa
kuwa Mahakimu.
“Toeni kipaumbele kwenye mashauri
ya Mirathi, Ndoa na Kuasili mtoto kwani mashauri haya huathiri hata malezi ya
watoto”, alisema Jaji Kiongozi.
Jaji Feleshi pia
aliwataka Mahakimu hao kuwa na kuendelea kuwa na uhuru katika kukosoa, kuandika
na kufanya utafiti. Aliwashauri Mhakimu hao kujiendeleza kielimu ili kuendana
na wakati kwa kuwa mambo mengi ya sasa yanabadilika kwa haraka.
Aidha, Jaji Kiongozi
aliwasisitiza Mahakimu hao kutekeleza majukumu yao kwa bidi na kuona umuhimu wa
kujiepusha na mambo yote yasiyofaa na yanayokinzana na maadili ya kazi yao na y
a Utumishi wa Umma.
Wakati
huo huo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar
es salaam Mhe. Lameck Mlacha amewataka Mahakimu hao kuandika Mwenendo wa shauri
pamoja na hukumu kwa ubora unaostahili.
Jaji Mlacha pia amewataka
Mahakimu hao kuwa makini utakapofikia wakati wa kuanza kusikiliza mashauri
yanayohusu uchaguzi Mkuu na pia kutenda haki katika kusikiliza mashauri hayo.
Aidha aliwataka kutotumia lugha zisizofaa katika kazi zao na kuhakikisha
wanakuwa ni Mahakimu wa mfano wa kuigwa katika utumishi wao.
Naye
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Leonard Magacha
akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania aliwataka Mahakimu
hao kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu za kazi ili kuleta ufanisi na tija
katika kazi.
Jumla ya Mahakimu wakazi
Daraja la kwanza 53 wamepangiwa vituo vya kazi (Mahakama za Hakimu Mkazi na
Mahakama za wilaya) baada ya kumaliza Mpango Maalumu wa kufanya kazi kwenye
Mahakama za Mwanzo na wilaya. Mahakimu hawa ni wale waliokuwa wasaidizi wa
kisheria wa Waheshimiwa Majaji ambao hivi karibuni waliapishwa kuwa Mahakimu.
Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya wakiwa kwenye kikao kazi chao. Hawa ni wale waliokuwa Wasaidizi wa Kisheria wa Waheshimiwa Majaji ambao waliapishwa kuwa Mahakimu hivi karibuni.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya alipofungua kikao kazi chao.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam Mhe. Lameck Mlacha akizungumza na Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya kwenye kikao kazi chao.
Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya wakiwa kwenye kikao kazi chao
Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya wakiwa kwenye kikao kazi chao
Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joseph Fovo (wa pili kushoto) na Messeka Chaba (kulia) wakiwa kwenye kikao kazi cha Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za wilaya. Katikati ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Desdery Kamugisha.
Asante
JibuFuta