Na Lydia Churi -Mahakama
Mwili wa
aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe.
Salvatory Benedict Bongole unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne tarehe 21/7/2020
katika kijiji cha Shimbi Kati wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mwili wa
Marehemu Jaji Bongole uliagwa jana katika Ibada iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa
wa Ikulu, Cheyo A mkoani Tabora na baadaye kusafirishwa kwenda wilayani Rombo
kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Jumanne.
Marehemu Jaji Salvatory
Bongole alifariki dunia Jumatano usiku, Julai 15, 2020 baada ya kuugua ghafla
nyumbani kwake.
Wasifu wa Marehemu Jaji Salvatory
Bongole
Marehemu Jaji Bongole
alizaliwa tarehe 6/4/1964 katika Kijiji cha Shimbi Kati Wilaya ya Rombo mkoani
Kilimanjaro Tanzania. Januari 1975 hadi Novemba 1981 alisoma shule ya Msingi
Kwandele.
Alijiunga na
masomo ya sekondari Uru Seminari kuanzia mwaka 1982 hadi 1985 alipohitimu
kidato cha nne. Mnamo Mei 1988 hadi Juni1989 aliendelea na masomo ya kidato cha
tano hadi cha sita UrU Seminari na Juni 1988 hadi Juni 1989 alijiunga na Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro na Makuyuni.
Septemba 1989
alijiunga na Chuo kikuu Dar es salaam akisoma Shahada ya kwanza ya Sheria na
kuhitimu Juni 1993.
Mnamo
10/6/1994 Mhe. Jaji Bongole aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania kama Hakimu
Mkazi Daraja la III.
Tarehe
16/10/2000 aliteuliwa kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Mtwara. Mnamo tarehe
2/8/2000 aliteuliwa kuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Mkoa wa Mtwara
kwa kipindi cha Miaka mitatu (3).
Tarehe
1/7/2001 alipandishwa cheo na kuwa Hakimu Mkazi Daraja la II.
Mnamo tarehe
25/2/2002 alihamishiwa Mkoa wa Iringa akitokea Mtwara kama Hakimu Mkazi wa Mkoa
huo. Tarehe 27/10/2004 aliteuliwa kuwa Hakimu Mkazi Daraja la I.
Tarehe
20/6/2006 aliteuliwa kuwa Msajili wa Wilaya Mahakama Kuu. Tarehe 14/11/2006
alipandishwa cheo na kuwa Hakimu Mkazi Mkuu daraja II.
Tarehe
9/5/2007 alihamishiwa Tabora kama Msajili wa Wilaya. Mnamo Tarehe 29/9/2009
aliteuliwa kuwa Hakimu Mkazi Mkuu daraja la I. Na mnamo tarehe 29/7/2010
alihamishiwa Mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam akitokea Tabora.
Tarehe
15/7/2010 aliteuliwa kuwa Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mnamo tarehe 15/6/2012 akiwa Naibu Msajili Mwandamizi aliteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania akapangiwa kuhudumu Divisheni ya Ardhi, baadaye tarehe
5/3/2013 alihamishiwa Masjala Kuu.
Tarehe 25/5/2016
aliteuliwa kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Bukoba. Tarehe 10/7/2018
alihamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Tabora akiwa ni Jaji Mfawidhi wa
kanda hiyo hadi mauti yalipomfika tarehe 16/7/2020.
Mwili wa
Marehemu Jaji Salvatory Bongele utazikwa nyumbani kwao Rombo, Kilimanjaro siku
ya Jumanne Tarehe 21/72020.
BWANA AMETOA NA BWANA
AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Waheshimiwa Majaji waliohudhuria Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole wakiwa mbele ya Jeneza.
Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora wakiwa kwenye Msiba wa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. Salvatory Benedict Bongole.
Familia ya Marehemu Jaji Salvatory Benedict Bongole.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu.
Waheshimiwa Majaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole.
Waheshimiwa Majaji wakiwa Msibani.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni