Na Innocent Kansha -Mahakama, Rombo
Mwili wa
aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe.
Salvatory Benedict Bongole umezikwa leo mchana katika kijiji cha Shimbi Kati wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ameongoza Waheshimiwa Majaji pamoja na Watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania katika mazishi hayo.
Marehemu Jaji Salvatory
Bongole alifariki dunia Jumatano usiku, Julai 15, 2020 baada ya kuugua ghafla
nyumbani kwake. Mwili wake ulisafirishwa siku ya Jumamosi Julai 18 baada ya Misa iliyofanyika nyumbani kwake,
Mtaa wa Ikulu, Cheyo A mkoani Tabora.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakibeba Jeneza lenye mwili wa wa aliyekuwa Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole kuelekea kwenye kaburi atakalizikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Shimbi Kati Rombo
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiingiza kaburini Jeneza lenye mwili wa wa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole.
Kaburi atakalizikwa Marehemu Jaji Bongole nyumbani kwao kijiji cha Shimbi Kati wilayani Rombo
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kulia) akiwa na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Kaburi la aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni