Ijumaa, 24 Julai 2020


         
                                  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA

                                       SALAAM ZA RAMBIRAMBI                                                                                                                                                                                                         
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amemtumia salaam za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.

Kufuatia kifo cha Rais Mstaafu, Mahakama ya Tanzania inaungana na Mhe. Rais, Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na watanzania wote kwa ujumla katika kuomboleza msiba mkubwa uliolipata Taifa letu.

Marehemu Mkapa atakumbukwa pia kwa kuunda Tume ya Rais ya Kero za Rushwa (Ripoti ya Warioba ya mwaka 1996) ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuipa Mahakama ya Tanzania na sekta ya sheria kwa ujumla, dira ya kupambana na Rushwa hadi leo hii.

Ni masikitiko makubwa kumpoteza Kiongozi mwenye upeo wa mbali, ambapo Mwaka 2000 alisimamia kutayarishwa kwa DIRA YA MAENDELEO 2025. Dira ambayo mwaka 2020 imeifikisha Tanzania kuwa Taifa lenye kipato cha kati.


“TUNAMTAKIA PUMZIKO LA AMANI RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILLIAM MKAPA”

Imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
MAHAKAMA YA TANZANIA



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni