Jumamosi, 5 Septemba 2020

WASAJILI NA MAHAKIMU WATAKIWA KULINDA AMANI YA NCHI

Na Lydia Churi-Mahakama, Morogoro

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Dkt. Paul Kihwelo amewataka Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi kutoa haki kwa wote kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizopo ili kulinda amani ya nchi.

Akifunga mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa baadhi ya Naibu Wasijili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi leo mjini Morogoro Jaji Kihwelo amesema kwa kuzingatia hayo, wananchi na wadau wengine wa Mahakama watajenga imani kwa Mhilimi huo na pia kujenga ujasiri wa kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika utoaji haki.

Jaji Kihwelo alisema endapo Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi hao watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ni wazi kuwa wataepusha migongano ya kimaslahi inayoweza kuifanya Mahakama kuonekana haipo huru.

“Lazima tutambue umuhimu wetu kama watoa haki, hivyo tumieni mafunzo mliyopata ili kuleta ufanisi na tija katika kusikiliza mashauri ya uchaguzi na yasiyokuwa ya uchaguzi” alisema Jaji Kihwelo.

Alisema Mahakama kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto imeandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuwaandaa Majaji, Wasajili na Mahakimu kutekeleza wajibu wa Mahakama katika tukio muhimu la uchaguzi Mkuu kwa manufaa ya taifa.

Mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kwa nyakati tofauti yanawahusisha Maafisa wa Mahakama wa ngazi mbalimbali wakiwemo Majaji, Wasajili, Mahakimu na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akifunga mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa Naibu Wasajili na Mahakimu wakazi jana mjini Morogoro.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akimkabidhi cheti Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakam ya Hakimu Mkazi Shinyanga Mhe. Mary Peter Mrio baada ya kumaliza mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa Naibu Wasajili na Mahakimu wakazi jana mjini Morogoro.

Naibu Wasajili wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akimkabidhi cheti Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara Mhe. Magdalena Ntandu baada ya kumaliza mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa Naibu Wasajili na Mahakimu wakazi jana mjini Morogoro.


 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni