Na Tawani Salum, Mahakama
Bodi ya Udhamini
wa Taarifa ya Majuzuu ya Sheria imeendelea kwa kasi kukamilisha uchambuzi wa maamuzi ya Juzuu la mwaka 2016 na majuzuu ya miaka ya nyuma kuanzia mwaka
2007 na kuendelea na ifikapo mwisho wa mwezi Oktoba mwaka huu inategemea kukamilisha
uchapishaji wa juzuu ya sheria ya mwaka huu.
Akizungumza katika
kikao cha Bodi hiyo, kilichofanyika hivi karibuni katika
ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi, Jaji
wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Jacobs Mwambegele alisema kuwa Majuzuu ya
mwaka 2007 hadi 2015,2017 ,2018 na 2019 tayari yamewasilishwa kwa Mzabuni kwa hatua ya mapitio na uchapishaji.
“Ni
mpango wa Bodi na Mahakama kuhakikisha
imemaliza kuchapisha Taarifa za Majuzuu ya Sheria ya Mwaka 2007
hadi Mwaka 2020 katika kipindi cha miezi kumi kuanzia mwezi wa nane mwaka huu,”
alieleza Mhe. Jaji Mwambegele.
Naye Kaimu Mratibu wa Bodi ya
Udhamini wa Taarifa ya Majuzuu ya Sheria, Mhe. Kifungu Mrisho Kariho alisema kuwa Bodi hiyo
imedhamiria kutoa Majuzuu hayo kwa mkupuo kwa kuwa tayari kipindi kirefu kimepita toka 2006 bila Majuzuu hayo kuwafikia wadau walaji na kurahisisha
tafiti za kisheria na kumalizika kwa Mashauri kwa wakati kupitia Wahe. Majaji
na Mahakimu.
Mhe. Kariho aliongeza kuwa Majuzuu hayo yatasaidia
katika uwasilishwaji wa hoja mpya za
kisheria Mahakamani kupitia Mawakili wa Serikali, Mawakili wa Kujitegemea pamoja na wadau wengine katika fani ya Sheria.
Bodi hiyo ina
jumla ya Wajumbe 12, ambao ni Majaji kutoka Mahakama ya Rufani, Majaji wa
Mahakama Kuu Tanzania Bara na Zanzibar, Wawakilishi toka Tanzania
Bara na Zanzibar, Katibu na Mratibu wa Bodi hiyo.
Pichani ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Udhamini ya Taarifa ya Majuzuu ya Sheria ambaye pia ni Jaji
wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Jacobs Mwambegele na kulia ni Katibu wa Bodi hiyo, Prof. H.I. Majamba
wakiwa katika kikao cha Bodi ya Udhamini ya Taarifa ya Majuzuu ya Sheria kilichofanyika hivi
karibuni.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Udhamini
ya Taarifa ya Majuzuu ya Sheria wakiwa katika kikao hicho, Kulia ni
Mhe.Jaji F. Manyanda, kushoto ni Bi. Nelly Mwasongwe na
katikati ni Bw. H.A. Haji.
Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Taarifa ya Majuzuu ya Sheria wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. S.A. Lila, katikati Ni Jaji wa Mhakama Kuu Zanziabr Mhe. A. Mwampashi na wa kwanza kulia ni ni Kaimu Mratibu wa Bodi hiyo Mhe.Kifungu Mrisho Kariho wakifuatilia kikao hicho.
Wajumbe wa Bodi hiyo wakiendelea na majadiliano, kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Ignas Kitusi na kulia ni Prof. Majamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni