Na Innocent Kansha - Mahakama
Jaji
Mfawidhi Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Sophia
Wambura amewataka watumishi wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano
na uadilifu ili kuleta tija kwa Taasisi.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi iliyofanyika katika
Mahakama hiyo Oktoba 23 mwaka huu, Mhe. Jaji Mstaafu Wambura alisema kufanya
kazi kama kama timu kutawezesha malengo yao na ya Taasisi kutimia.
“Ili
mkono ukamilike ni lazima kila kidole kiwepo, ndipo mkono unaweza kufanya kazi
kwa ukamilifu na ufanisi ndivyo basi tunatakiwa kama watumishi kufanya kazi kwa
ushirikiano na kufikia mafanikio kwa maslahi mapana zaidi”, alisema Jaji .
Jaji
Wambura aliongeza kwa kuzungumzia nafasi ya kiongozi katika kufanikisha hilo
huku akisema kuwa. “Kiongozi bora ni mtu anayetumia muda wake kuonyesha dira ya
kuwafikisha Watu kwenye hatima ya mafanikio ya mtu moja moja na hata Taasisi
anayoiongoza kwa kusimamia uwazi, uwajibikaji na mahusiano mazuri pahala pa
kazi.”
Aidha,
Mhe. Jaji Mstaafu Wambura aliwaeleza watumishi hao kuwa katika kutimiza
majukumu yao ni lazima waige kundi la ndege warukao angani bila kuongozwa na
mtu bali hutumia karama walionayo na kufikia hatima yao kwa juhudi na
ushirikiano wao. “Kila Mtumishi aliyepo hapa yupo kwa sababu na si bure hivyo
anatakiwa kuonyesha karama ulizonazo kwa kushirikiana na wengine ili malengo
yenu kama Watumishi na Taasisi yenu yatimie.”
Jaji
Wambura aliwakumbusha watumishi kuzingatia maadili ya kazi ili kutoharibu
taswira ya Taasisi na kupoteza imani ya Umma unaouhudumia, Viongozi wanapaswa kutoa
maelekezo ya mara kwa mara kuwakumbusha watumishi masuala muhimu ya kinidhamu.
Kwa
upande mwingine, Mhe. Jaji Wambura aliwataka Watumishi kutoridhika na nafasi
zao kazini aliwaasa kutafuta njia mbalimbali za kuongeza na kujiendeleza
kielimu ili kutafuta fursa zaidi na kupanua wigo wa ujuzi na umahiri ili
kutimiza majuku yao kwa ufasaha na weledi mkubwa zaidi.
Awali
akitoa neno la utangulizi kwa niaba ya watumishi, Kaimu Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Devisheni ya Kazi, Mhe. Imani Daud Aboud alisema kuwa
wangependa kuendelea kuwa na Jaji Mstaafu Wambura kwa ari ya utendaji kazi wake
ila kwa mujibu wa sheria hana budi kupumzika katika utumishi.
Mhe.
Jaji Aboud aliongeza kuwa Jaji Mstaafu Wambura ni mtu aliyekuwa na upendo wa
hali ya juu kazini, ushirikiano, kusimamia nidhamu za watumishi, alikuwa mtiifu
na mwadilifu, aliongeza kuwa alikuwa mpenda haki asiye na makuu na lionyesha
unyenyekevu siku zote na kiongozi hodari.
Naye,
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Zainab Muruke
alimuelezea Jaji Mstaafu Sophia Wambura kama mfanyakazi hodari mwenye msimamo
imara wa kusimamia mambo anayoyaamini katika kazi, kuwatia hari watumishi hasa
wa jinsia ya kike na kuwaasa watumishi kutobweteka kujiendeleza kitaaluma ili
kuboresha ufanisi kazini
Jaji
Mstaafu Sophia Wambura amestaafu baada ya kuhutumikia Muhimili wa Mahakama kwa
takribani miaka 35 katika nyadhifa mbalimbali.
Jaji
Mfawidhi Msataafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Sophia
Wambura (aliyesimama) akitoa nasaha zake kwa watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni
ya kazi wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama hiyo
Jijini Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe Imani Daud Aboud na kushoto ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Zainab Muruke.
Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Imani Aboud (aliyesimama) akitoa neno la utangulizi wakati wa Hafla ya kumuaga Jaji
Mfawidhi Msataafu, Mhe. Sophia
Wambura (wa pili kulia), kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Divisheni ya Kazi, Mhe. Zainab Muruke na wa kwanza kulia ni Mtendaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi- Bi. Hellen Mkumbwa.
Jaji
Mfawidhi Mstaafu, Mhe. Sophia Wambura
(wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi (wa pili kushoto) ni Kaimu Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania- Divisheni ya Kazi Mhe, Imani Aboud,
(wa kwanza kulia) ni Jaji wa Divisheni hiyo, Mhe.
Zainab Muruke na (wa kwanza kushoto) ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania- Divisheni ya Kazi Mhe. Angaza Mwipopo.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Zainab Muruke (aliyesimama)
akitoa neno la shukrani mbele ya Jaji Mfawidhi Msataafu, Mhe. Sophia Wambura wakati wa hafla ya kumuaga
iliyofanyika katika Ukumbi wa Mahakamani hapo, kushoto ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Angaza Mwipopo.
Mtumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Bi. Jane Lwiza kwa niaba ya watumishi wenzake akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Mstaafu, Mhe. Sophia Wambura.
Baadhi
ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi wakifanya Igizo fupi
la kupanga mbinu za kukabiriana na adui kama ishara ya kuonyesha maana ya
uongozi mahala pa kazi wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Mfawidhi Msataafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi Mhe. Sophia
Jaji
Mfawidhi Msataafu Mhe. Sophia
Wambura akikata Keki iliyoandaliwa na watumishi wa Mahakama Divisheni ya Kazi ikiwa ni ishara ya kumpongeza baada ya kustaafu utumishi rasmi.
Hongera sana Mhe. Jaji Sophia Wambura Mama mwenye busara na maadili mema kwa wote. Katika uongozi wako nikikumbuka ukiwa Msajili Mahakama kuu ya Tanzania Mbeya. Ulionyesha upendo kwa watumishi bila ubaguzi. Na uliendelea hata ulipokuwa Mhe. Jaji kwa kujituma na kuwahamasisha watumishi ngazi zote,wahe. Mahakimu na Wahe. majaji na kuenzi maadili ya kazi na imani katika dini zote. Ninakupongeza kwa utumishi uliotukuka Mhe. Sophia Wambura. Mungu akulinde na akutunze daima. Akujalie afya njema na kuufikia uzee mwema na mkamilifu. Ninakupenda Mama. ❤
JibuFuta