Na Lydia Churi- Mahakama Mwanza.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ameiomba
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kusaidia upatikanaji
wa gereza lingine katika wilaya hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa
wananchi.
Akizungumza
na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Emmanuel Kipole pamoja na Kamati ya Ulinzi na
Usalama, Jaji Kiongozi amesema bila ya kuwa na mkakati madhubuti wa kuhakikisha
kunakuwa na gereza lingine Sengerema, ni wazi mashauri hayatamalizika kwa
wakati mahakamani.
Alisema
katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, Mahakama ya wilaya
ya Sengerema ilisajili mashauri 329 na kati ya hayo, mashauri 325 yaliamuliwa
na yaliyobaki yaklikuwa ni 118. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya mashauri kubaki
ni kukosekana kwa magereza kwenye wilaya hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo iliyosomwa kwa Jaji
Kiongozi, mahabusu hufikishwa mahakamani mara mbili kwa wiki kwa ajili ya
kusikilizwa kwa mashauri yao hali inayosababisha mashauri kutokumalizika kwa
wakati.
Akizungumza
na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita pamoja na Mahakama ya wilaya ya
Sengerema kwa nyakati tofauti, Dkt. Feleshi aliwataka watumishi hao kujiepusha
na vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili, kuacha kuchongeana pasipokuwa na sababu za msingi na
kuchafuana, badala yake wathaminiane na kuheshimiana kila moja katika kada
yake.
Aliwataka
watumishi hao kujiendeleza kielimu kwenye kada nje ya kada walizoajiriwa ili
kuongeza ujuzi wa masuala mbalimbali. “Tujitahidi kujenga uwezo na thamani
yetu, tusifanye kazi kwa mazoea” alisema.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alielezea changamoto inayotokana
na ukubwa wa wilaya yake kwamba wananchi wengine wamekuwa wakisafiri umbali
mrefu kufuata huduma za Mahakama makao makuu ya wilaya hiyo.
Alisema
wilaya ya Sengerema inazo Tarafa 2 na kata 47 ambapo kata 5 kati ya hizo zipo
maeneo ya visiwani umbali wa zaidi ya kilometa 100 kutoka makao makuu ya wilaya
hiyo hivyo wananchi wengine hutumia gharama kubwa kufuata haki zao.
Aidha
Mkuu huyo wa wilaya alimshukuru Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis
Juma pamoja na viongozi wengine wa Mahakama kwa kusikia ombi lao na kuwaongezea
idadi ya Mahakimu watatu katika Mahakama ya wilaya ya Sengerema. Awali Mahakama
hiyo ilikuwa na Hakimu moja tu.
Kuhusu
ombi la Mkuu wa wilaya ya Sengerema la kuanzishwa kwa Mahakama ya pili ya
wilaya kwenye wilaya hiyo, Jaji Kiongozi alisema Mahakama ya Tanzania
itaangalia uwezekano wa kuanzisha masjala ndogo ya Mahakama ya wilaya ili
kusogeza huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Jaji
Kiongozi anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Geita ambapo atamalizia katika
wilaya za Bukombe na Chato.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ya Sengerma wakati wa ziara ya Jaji Kiongozi kwenye kanda hiyo.
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (katikati waliokaa).
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akimsikiliza Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita akielezea jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (hayupo Pichani) wakati Jaji Kiongozi alipomtembelea ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi wakati Jaji Kiongozi alipomtembelea ofisini kwake.
Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita pamoja na Viongozi wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi mara baada ya kuzungumza nao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni