Na Festo Sanga, Mahakama-Kigoma
Jumla
ya Mahakimu na Maafisa 40 wa kada mbalimbali wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma wamepatiwa
mafunzo ya Uongozi ili kuwajengea uwezo watumishi hao kuweza kuimarisha maadili
na umalizaji wa mashauri haraka kwa viwango ambavyo Kanda imejiwekea.
Akifungua
rasmi mafunzo hayo hivi karibuni yaliyofanyika Wilayani Kibondo-Kigoma, Jaji
Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. Jaji Ilvin
Mugeta alisema lengo ni kuhakikisha kwamba watumishi wa ngazi ya Maafisa wa
Mahakama na wale wa utawala (judicial and non- judicial officers) wanapata
mafunzo katika maeneo ya Uongozi, Maadili, ukaguzi, usimamizi wa
mashauri na usimamizi wa mali za Umma.
“Natambua baadhi yenu hususani Mahakimu wa Mahakama za mwanzo lakini pia
maafisa mbalimbali ni waajiriwa wa siku za karibuni, ndio maana tumeendaa
mafunzo haya ili kuwajengea uwezo kiuongozi ili muweze kutekeleza majukumu yenu
kwa weledi na ufanisi na kujenga imani kwa walio chini yenu’ alisema Jaji
Mugeta.
Jaji
Mugeta aliongeza kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa Watumishi hao yamelenga pia
kuwawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiutumishi na hatimaye
watumishi wanapofika kwa viongozi hao wawe na imani ya kupata suluhu ya matatizo yao.
“Hakuna
kitu kibaya kama kuongoza watumishi wasio na furaha, hivyo ni wajibu wa
kiongozi kurejesha furaha ya watumishi kwa kuwasikiliza na kuwaongoza vyema,” alisisitiza
Jaji huyo Mfawidhi.
Hata
hivyo, Jaji Mugeta alieleza kuwa
Mahakama kanda ya Kigoma inayo maeneo mahsusi katika utekelezaji wa kila siku wa mipango na
shughuli ambayo usimamizi wake ni kipaumbele cha kwanza, huku akiyataja maeneo
hayo kuwa ni kuimarisha maadili na umalizaji wa mashauri haraka kwa viwango
ambavyo Kanda imejiwekea.
Naye
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Bw. Moses Mashaka alisema katika utekelezaji wa mpango wa Mafunzo ya
ndani kwa mwaka 2019/2020 na mpango wa mafunzo wa mwaka 2020/2021 jumla ya
watumishi 83 wa kada mbalimbali walipewa mafunzo.
Bw.
Mashaka alisema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Kanda hiyo ilitoa mafunzo juu ya taratibu za kufungua mashauri, maadili ya utumishi
wa Umma, usimamizi na ujazaji sahihi wa rejesta za mashauri, mpango mkakati wa
Mahakama na mfumo wa kuratibu mashauri(JSDS
II), Miongozo mbalimbali kuhusu usimamizi wa watumishi, usimamizi wa mashauri,
na usimamizi wa Magari.
“Mafunzo
hayo yameleta mabadiliko yenye tija katika utendaji kazi kwa mtumishi mmoja
mmoja na kanda kwa ujumla” alisema Bw. Mashaka.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Kigoma, Mhe. Jaji Ilvin Mugeta akifungua mafunzo ya Uongozi kwa
Mahakimu na Maafisa wa kada mbalimbali yaliyofanyika wilayani Kibondo hivi
karibuni.
Mtendaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Kigoma, Bw. Moses Mashaka akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa
mafunzo ya ndani kwa washiriki wa mafunzo.
Mhe. Jaji Mfawidhi
akiwasilisha mada ya Uongozi kwa washiriki wa mafunzo.
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada ya Uongozi iliyotolewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni