Uongozi
wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bwn.
Jumanne Omar Mbonde aliyekuwa Mlinzi Mwandamizi wa Mahakama ya Mwanzo Ikwiriri
wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Bwn.
Mbonde alifariki Dunia jana tarehe 19/11/2020 katika kituo cha Afya Ikwiriri alipokuwa
akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa shinikizo la Damu.
Mwili wa Marehemu Mbonde umezikwa leo Rufiji
mkoani Pwani.
Marehemu
Jumanne Mbonde alizaliwa Aprili 20 mwaka 1968 wilayani Rufiji na baadaye aliajiriwa
na Mahakama ya Tanzania Oktoba 1 mwaka 2004 kama Mlinzi. Hadi mauti inamfika,
Marehemu alikuwa ni Mlinzi Mwandamizi.
Inna Lillah
wa Inna layhi Rajiun.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni