Na Stanslaus Makendi, Mahakama Kuu - Dodoma
Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mheshimiwa Latifa
Mansoor amewataka Mahakimu wa Kanda hiyo kujiimarisha katika matumizi ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kurahisisha usikilizwaji wa mashauri
mahakamani na upatikanaji wa haki kwa wakati.
Akizungumza
wakati wa hafla ya ya ugawaji wa Kompyuta Mpakato (Laptop) zilizotolewa na
Mahakama ya Tanzania kwa Mahakimu wote nchini, Jaji Mansoor aliwataka Mahakimu
hao kuvitunza vizuri vitendea kazi hivyo na kuhakikisha vinatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa pekee.
Mahakama
ya Tanzania kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati wake pamoja na mradi wa Maboresho
ya huduma za Mahakama imewapatia Mahakimu wote nchini Laptops kwa ajili ya
kuboresha utendaji kazi wao kama hatua ya utekelezaji wa Mpango mkubwa wa
kutoa huduma za kimahakama kwa njia ya mtandao (e-judiciary) na hatimaye haki
mtandao (e-justice).
“Vifaa
hivi ni vitendea kazi vya ofisi, hivyo tunatarajia vitaleta tija katika kazi
zetu na hatimaye kuimarisha imani ya wananchi juu ya utendaji wa Mahakama,
alisema Kaimu Jaji Mfawidhi huyo”
Mahakama
za Mkoa wa Dodoma zimepatiwa jumla ya kompyuta sitini (60), mashine kubwa ya
kudurufu nyaraka moja (1) na ‘Scanner’ tisa (9) ambazo zimegawiwa kwa Mahakama
zote ndani ya Mkoa huo kuanzia Mahakama Kuu na Mahakama zote za chini
Mahakama
ya Tanzania imetoa vifaa hivyo kwa Mahakama zote nchini kwa lengo la kuboresha
utendaji kazi na ufikiwaji wa lengo la utoaji wa haki kwa wakati kwa wananchi.
Vifaa hivyo vinatarajiwa kuongeza kasi ya utoaji na upatikanaji wa nyaraka za
maamuzi yanayotolewa na Mahakama katika ngazi mbalimbali za Mahakama nchini
ikiwemo nakala za hukumu, mienendo ya mashauri na amri mbalimbali za
kimahakama.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mheshimiwa Latifa Mansoor akimkabidhi moja wa Mahakimu kitendea kazi (Laptop)
Mahakimu wa kanda ya Dodoma wakizungumza na Kaimu Jaji Mfawidhi wa kanda hiyo Mhe. Latifa Mansoor.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni