Ijumaa, 5 Februari 2021

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA HAI MOSHI AFARIKI DUNIA

 

 Marehemu Alodia Leonard Rwechungura

TANZIA

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Jaji Beatrice Mutungi anasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi, Bi. Alodia Leonard Rwechungura pichani aliyekuwa akifanya kazi katika Mahakama ya Wilaya Hai kama Katibu Mahsusi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kanda hiyo, Marehemu Alodia alikutwa na umauti Februari Mosi, 2021 katika hospitali ya Kibong'oto Wilayani Hai.

Mazishi ya marehemu yamefanyika Bukoba mjini mkoani Kagera Februari 04, 2021. Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni