Jumatano, 3 Februari 2021

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA JAJI GALEBA KUWA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI (T)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mhe. Jaji Zephrine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika mapema Februari 02, 2021 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, huku ikishuhudiwa na viongozi kadhaa wa Mahakama na Serikali ikiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Katiba na Sheria, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu wa Mahakama, DPP, Wakili Mkuu wa Serikali na wengineo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akimuapisha Mhe. Zepharine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania
kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino  Februari 2, 2021.
Mhe. Zephrine Nyalugenda Galeba akila kiapo .

Kamishna wa Maadili Jaji Siiyangilwa Sikalilwa Mwangesi akimlisha

kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Zephrine Nyalugenda Galeba
aliyeapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania
kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Februari 2, 2021.

Mhe. Rais akizungumza mara baada ya kumuapisha Mhe. Jaji Galeba.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni