JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA,
MENEJIMENTI NA WATUMISHI WOTE WA MAHAKAMA WANAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUOMBOLEZA
MSIBA HUU MZITO ULIOTUPATA KUFUATIA KIFO CHA RAIS WETU WA JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.
KUFUATIA MSIBA HUU, MAHAKAMA YA TANZANIA INATOA SALAAM
ZA POLE KWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMA SAMIA SULUHU
HASSAN PAMOJA NA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI.
RAIS MAGUFULI ATAKUMBUKWA KWA MCHANGO WAKE ALIOUTOA
KWA MAHAKAMA IKIWEMO KUIMARISHA MIUNDO MBINU YA MAHAKAMA NA MAPAMBANO DHIDI YA
RUSHWA KWA KUWEZESHA UANZISHWAJI WA DIVISHENI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU
UCHUMI YA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli (enzi za uhai wake) akiwa na Rais wa Jamhuri ya Burundi,
Mhe. Evariste Ndaishimiye (wa pili kulia) pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi
rasmi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Kigoma Septemba 19, 2020.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni