Na Innocent kansha – Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ahaidi kutoa waraka kwa Maafisa wote wa Mahakama
ya Tanzania kutoa taarifa za wazi zitakazosaidia kurahisisha shughuli za Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini kushughulikia masuala baina ya Tume na
Mahakama.
Akizungumza na ujumbe wa
tume hiyo iliyomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam Machi 17, 20201
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Juma alisema, nawakikishia kutao ushirikiano
kwa masuala yahusuyo Mahakama katika kushughulikia kero za wananchi.
“Tuishukuru serikali kwa
kutambua changamoto za Mahakama na kwa kiasi kikubwa zimefanyiwa kazi,
maboresho haya makubwa yaliyofanyika ni kutokana na mpango mkakati wetu wa
miaka mitano 2015/16 hadi 2020/2021 umesaidia kuainisha sehemu zenye changamoto
kubwa zaidi na kuzifanyia kazi”, aliongeza Jaji Mkuu.
Aidha, Prof. Juma
alieleza kuwa amepokea ombi la tume lakutaka kupewa mafunzo na elimu kuhusiana
na mabadiliko na maboresho makubwa yanayoendelea mahakamani ili iweze
kuwasaidia Tume kuwashauri wateja wao ipasavyo.
Jaji Mkuu aliongeza kuwa
matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli za
utoaji haki imeonyesha mafanikio makubwa hususani kipindi cha mwaka wa jana
2020 wakati wa ugojwa wa Corona Mahakama iliweza kusikiliza kesi nyingi za
jinai kushinda wakati wowote wa usikilizwaji wa mashauri hayo.
“Ndoto yangu
nikuona tunatumia teknolojia ya TEHAMA ili mahakama zetu zitumimike kutoa
taarifa zote muhimu zinazohusu mashauri na huduma zitolewazo kumsaidia
mwananchi anaefika kupata huduma mahakamani bila kubabaika kwani mfumo huu ni
huru na wawazi zaidi”, alisisitiza Jaji Mkuu.
Alikadhalika, Jaji Mkuu aliueleza ujumbe wa
tume kuwa, Mahakama inautaratibu wake wa kujitathimini kupitia taasisi binafsi
kama REPOA kila baada ya miaka mitano ili kutathini utendaji kazi na kiwango
cha kuridhishwa watumiaji wa huduma za Mahakama.
Jaji Mkuu pia,
aliwapongeza Mwenyekiti wa Tume na Makamishina wote kwa kuteuliwa kwao kushika
nyadhifa hizo.
Naye, Mwenyekiti wa Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu ameipongeza
Mahakama kwa jitihada zake za kuimarisha mfumo wa utoaji haki nchini matharani
kuongeza idadi ya majengo ya mahakama kwa ngazi zote za kimahakama, matumizi ya
TEHAMA katika utoaji haki,Uandaaji wa miongozo mbalimbali inayotumika katika
uendeshaji wa mashauri mahakamani, matumizi ya Mahakama inayotembea ili
kuwahudumia wananchi kwa kusogeza huduma karibu zaidi pamoja na utoaji wa elimu
kwa umma juu ya shughuli za Mahakama kupitia vyombo vya habari.
Pia, Mwenyekiti wa Tume Mhe.
Mwaimu aliipongeza serikali kwakuongeza idadi ya rasilimali watu mahakamani
kama vile Majaji, Mahakimu na watumishi wa kada zingine hii ni kutokana na
ushauri wa busara wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Aidha, Mwenyekiti
aliipongeza Mahakama kwa hatua zinazoendelea za ujenzi wa makao makuu ya
Mahakama Jijini Dodoma ili kuhamishia shughuli zake rasmi.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti huyo aliishukuru Mahakama kwa kushirikiana na Tume katika kuisaidia serikali kuwahudumia wananchi wake mathalani utoaji wa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri bure, kuweka mipango mathubuti ya kutocheleweshwa kwa mashauri mahakamani na malipo ya mafao kwa watumishi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Msataafu Mhe. Mathew
Mwaimu (kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake, kulia ni Kamishna wa
Tume hiyo Mohamed Khamis.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni