Marehemu Salima Mohamed enzi ya Uhai wake
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha
Mtumishi wake Bibi Salima Mohamed aliyekuwa Mtunza kumbukumbu wa Mahakama ya
Mwanzo Ukonga kilichotokea jana tarehe 3//3/2021 nyumbani kwake Ukonga jijini Dar
es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Aidha, kufuatia kifo hicho, mwili wa marehemu
umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao wilayani Newala mkoani Mtwara kwa ajili
ya maziko. yanayotarajiwa kufanyika kesho, Ijumaa tarehe 5/3/2021.
Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa
familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni