Na Innocent Kansha, Mahakama – Lushoto
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Paul Faustine Kihwelo amewataka Mahakimu
Wakazi wapya kutenda haki kwa kufuata sheria, miongozo na ushahidi unaotolewa
mbele yao.
Akifungua
mafunzo elekezi ya awamu ya pili kwa Mahakimu Wakazi hao, Jaji Kihwelo ambaye
pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, akizungumza kwa niaba ya
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi alisema
Mahakimu wanapaswa kuamua kesi kwa kuzingatia sheria, ushahidi uliopo na miongozo
ya kimahakama na si vinginevyo,
Aidha,
Jaji Kiwhelo aliongeza kuwa hakuna uhuru usio na wajibu, na wajibu wao ni kutenda
haki kwa kufuata sheria, kuamua mashauri kwa kuzingatia viapo ambavyo
vinawataka kutenda haki pasipo kuangalia rangi, dini, chama, umri wala jinsia
ya mtu.
“Msiamue
mashauri hayo kwa chuki, huba, tetesi, hisia, kwa misukumo na mihemko
mbalimbali, nendeni mkawe muarobaini wa kutoa suluhisho kwenye maeneo ambayo
yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi katika Mahakama za Mwanzo”, alisisitiza
Jaji Kihwelo.
Aliyaelezea
maeneo hayo kuwa ni mashauri ya mirathi, mgawanyo wa mali za ndoa, matunzo na
hifadhi ya watoto pia kukazia na kutimiza hukumu. Alisema wajibu wa Mahakimu ni
kuwa makini na kuchukua tahadhali kubwa kwani maamuzi mabaya juu ya maeneo haya
huumiza makundi maalumu yanayohusisha wototo, wajane, wagane na wazee, na pia huondoa
imani ya wananchi kwa Mahakama.
Dkt.
Kihwelo, aliwakumbusha Maafisa hao wa Mahakama kujiepusha na vitendo
vinavyoweza kuharibu taswira ya Mahakama kama matumizi ya lugha chafu,
kujigeuza Mungu watu, mavazi yasiyozingatia maadili ya kazi, ufuska,
ubabaishaji, ulevi, kuchelewa kuanza Mahakama, kuingilia au kuhoji maswali
wakati kesi ikiendelea kwa kiwango cha kupitiliza, kuchelewesha maamuzi na
kutotoa nakala za hukumu. Mambo haya ni kinyume na maadili ya utumishi wa
Mahakama.
Aliwahimiza
kujinoa zaidi kwenye matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
na mifumo ya kielektroniki inayotumika mahakamani ili waweze kuendana na kasi
ya mabadiliko ya kidunia.
“Raha
ya kuwa Afisa wa Mahakama wa sasa ni pamoja na kuwa na ujuzi na uelewa wa
kutosha katika matumizi ya TEHAMA. Pia kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya
kuongeza tija na manufaa ya Mahakama na Taifa kwa ujumla.
Jaji
Kihwelo aliwataka Mahakimu hao kutojitenga na wananchi na mamlaka zinazoongoza
kuanzia ngazi ya mashina, Vijiji, Kata na Tarafa kwa kisingizio cha kulinda
Uhuru wa Mahakama. Viongozi wa maeneo haya husika ni walinzi wa amani na pia ni
wadau muhimu sana wa Mahakama.
Kuhusu
suala la kutoa hukumu kwa wakati, Jaji Kihwelo amewahimiza Mahakimu hao
kumaliza mashauri ndani ya muda usiozidi miezi mitatu na kuzingatia lengo la
kumaliza mashauri 260 kwa mwaka. Kwa kufanya hivyo watafikia lengo la kutenda
haki kwa wote na kwa wakati. Nawakumbusha kuchapa kazi zenu na kufunga
majalada, kuwasilisha katika Mahakama za juu majalada yanayoitishwa ama
kukatiwa rufaa.
Kwa
upande wake, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma
aliwakumbusha Maafisa hao kutambua nyadhifa zao na kujiepusha na vitendo vinavyoidhalilisha
Mahakama na hategemei kuona Afisa wake kwa namna yoyote akitenda matendo yasiyoendana
na kiapo chake.
“Tumieni
mamlaka ya uhakimu pale ambapo taratibu zinaruhusu na si vinginevyo”,
alisisitiza.
Naye,
Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Kevin Mhina aliwaasa Maafisa hao kuwa kazi
ya uhakimu haina mambo mengi zingatieni haya kusikiliza kesi, kuandika mwenendo
na kutoa maamuzi hivyo mkatende haki na kumaliza mashauri kwa wakati na kutoa
nakala za hukumu kwa wakati.
“Tunapozungumzia
suala la maadili watu wengi wanadhani ni rushwa na ulevi hata uendeshaji mbaya
wa kesi pia inachukuliwa kama utovu wa maadili”, aliongeza Mhe. Mhina
Jumla
ya Mahakimu Wakazi daraja la pili 70 waliapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Prof. Ibrahim Hamis Juma Februari 26, 2021 Jijini Dar es salaam na kufanya idadi
ya Mahakimu Wakazi wapya kufikia 140 walioapishwa katika kipindi cha wiki moja.
Baadhi
ya Mahakimu Wakazi wakifuatilia Mafunzo Elekezi yanayoendelea katika chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto.
Baadhi ya Mahakimu Wakazi wakifuatilia Mafunzo Elekezi yanayoendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto.
Msajili
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma akitolea ufafanuzi wa jambo
wakati wa mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi II wapatao 71 (hawapo pichani) yanayofanyika
Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni