Na Innocent Kansha – Mahakama Mwanza.
Mahakama ya Tanzania inajenga Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Buswelu Jijini Mwanza kitakachogharimu y ash. 8.5 Bilioni.
Kituo hicho kitajumuisha ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama Kuu pia Masjala ndogo ya Mahakama ya Rufani na Ofisi za Wadau muhimu wa Mahakama kiutendaji, ikiwemo mawakili wa Serikali na wa kujitengemea, Ustawi wa Jamii, Polisi, Magereza, waendesha mashtaka ili kurahisisha na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za haki kwa wadau wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kushuhudia ujenzi huo mnamo Mei
26, 2021, Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bw. Fabian Michael Kwagilwa alisema
jengo hilo litakuwa la ghorofa tatu na limezingatia Mazingira bora, yakisasa na
Rafiki katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimahakama (mifumo
mbalimbali inayotumia teknolojia ya kisasa)
Mhandisi Kwagilwa alisema vigezo vingini ni Kuingilika/kufikika kwa urahisi ndani ya jengo kwa wazee, walemavu, wanawake na watoto, (provision of ramps and lifts). Usalama kwa watumiaji wa Mahakama (Mahabusu, Raia, Wafanyakazi), Urahisi wa wananchi kufika kwenye jengo ili kupata elimu na taarifa mbalimbali kuhusu Mahakama.
Alisema kituo kituo hicho kilichoanza kujengwa Januari 24 mwaka jana ujenzi wake umefikia asilimia 58 na kinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2021 na kinatarijiwa kuanza kutumika ifikapo Desemba mwaka huu.
Mhandisi Kwagilwa alisema moja ya malengo ya msingi katika Mpango Mkakati wa Mahakama ni kuboresha miundombinu ya majengo ya Mahakama mijini na vijijini ili kutimiza azma ya kusogeza huduma za kimahakama karibu zaidi na wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa C.F Builders Limited wanaojenga kituo hicho, Bw. Ferdnand Chacha alisema watakamilisha ujenzi kwa wakati na kwa kiwango cha hali ya juu.
Katika zoezi zima la uboreshaji wa miundombinu ya majengo, utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama unaendelea katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuanzia Mahakama za mwanzo hadi Mahakama ya Rufani.
Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki kinachoendelea kujengwa Buswelu Jijini Mwanza, ikiwa ujenzi wake umefikia asilimia 58 na kinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2021
Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki kinachoendelea kujengwa Buswelu Jijini Mwanza, ikiwa ujenzi wake umefikia asilimia 58 na kinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2021
Mkurugenzi
Mtendaji wa C.F Builders Limited wanaojenga kituo hicho, Bw. Ferdnand Chacha
akifafanua mbele ya waandishi wa habari namna watakavyo jenga kwa wakati na kwa kiwango cha hali ya juu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni