Na Innocent Kansha – Mahakama Lushoto.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Salum Massati amefunga rasmi mafunzo elekezi ya wiki moja kwa Majaji saba wa Mahakama ya Rufani na kuwataka wakatumie ujuzi na maarifa waliojengewa na wakufunzi wakayatumie kufanya kazi kwa weledi na uadilifu watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao mapya.
Akizungunza wakati wa
kufunga mafunzo elekezi hayo katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto mnamo
Juni 4, 2021 Jaji Massati alisema, wengi wenu mmepitia changamoto nyingi na
mafanikio, mkajenga historia zenu za nyuma kiutendaji kwa mafanikio hicho ndicho
kimekuwa kigezo cha kuteuliwa kwenu kwenda Mahakama ya Rufani.
“Rudini mkatumie ujuzi
huu kule mtakapokwenda kufanya kazi zenu za kila siku, mnatakiwa kutumia muda
wenu kurejea hadidu za rejea ili ziwajengee uwezo wa kutoa maamuzi ya busara mara
zote mtakapotekeleza majukumu yenu”, alisema Jaji Massati.
Aidha, aliongeza kuwa siku
tano walizokaa darasani Majaji hao zinatosha kwa kupata muelekeo wa kutekeleza
majukumu yenu mapya kwani mambo mazuri hujitokeza mwishoni naamini mmepikwa na
kuiva vizuri kulingana na ratiba yenu na pia madhumuni ya mafunzo hayo elekezi mmeyahitimisha
kwa ufasaha.
Jaji Mstaafu Massati
alisema uwepo wenu kwenye mafunzo elekezi hayo sio tu umewajengea udugu mtakao
kuwa nao kwa muda mrefu muwapo kazini bali yamewajengea hekima na busara
mtakayo itumia wakati wote mtakapokuwa mkifanya maamuzi kwa mustakabali wa
ustawi wa Taifa.
Naye, Jaji wa Mahakama ya
Rufani Mhe. Patricia Fikirini alisema mafunzo haya elekezi ni muhimu sana
yametuelekeza mambo mengi na muhimu sana yametuvusha daraja muhimu kutoka ngazi
ya Mahakama Kuu na kutupeleka Mahakama ya Rufani.
“Wengi wetu tulipoona
uteuzi tulijiuliza maswali mengi sana na hata tulipokutana na Jaji Mkuu wa
Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya uteuzi hatukujua tunakwenda kujadili mambo
gani, sasa tumetambua kupitia mafunzo haya elekezi yametuvusha vema kutoka kujua
majukumu ya Mahakama Kuu na kutambua majukumu mapya ya Mahakama ya Rufani”,
Jaji Fikirini amewaomba
waandaaji wa mafunzo hayo kuyafanya kuwa endelevu hata kama sio hapo Chuoni
yaendelee kutolewa ili kuendelea kuwajengeza uwezo zaidi kuimarisha uwezo wao
zaidi kiutendaji, na wasisite kutoa ushirikianao pale watapowahitaji kufanya
hivyo.
Wakati huo huo, Jaji wa
Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama ya Lushoto
yalipokuwa yakiendeshwa mafunzo elekezi hayo Mhe. Dkt. Paul Faustine Kihwelo
alisema anawashukuru Majaji kwa kuonyesha utulivu, mshikamano, kuchangia majadiliano
na kujitoa kwao muda wote wa mafunzo.
“Kama mkufunzi unapofundisha
watu ukaona wamekaa kimya utajiuliza mengi, kama je? watu hao wamekuelewa au
hawajakuelewa kwenu Mhe. Majaji ilikuwa tofauti kabisa mafuzo yamekuwa ya
ushirikishwaji wa hali ya juu na hoja zote mmechangia kwa kiwango cha juu
nawapongeza sana”, aliongeza Mhe. Dkt. Kihwelo.
Jaji Dkt. Kihwelo
aliwataka radhi kwa mapungufu yaliyojitokeza hasa katika kipindi chote cha siku
tano kwa mapungufu yaliyojitokeza na kuwafanya kutokuwa watulivu muda wote wa
mafunzo elekezi hayo.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Salum Massati akizungumza na Majaji wa Mahakama ya Rufani (hawapo pichani) wakati alipofunga rasmi mafunzo elekezi ya siku tano ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto mnamo Juni 4,2021
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Patricia Fikirini akitoa nasaa zake wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Patricia Fikirini akitoa nasaa zake wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania
Baadhi ya Jaji wa Mahakama ya rufani wakifurahia jambo wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku tano Chuoni Lushoto
Jaji wa Mahakama Rufani ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto akipokea Cheti wakati wa kufunga Mafunzo elekezi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani yaliyoendeshwa kwa siku tano mnamo Juni 4, 2021 kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu wa Mahakam ya Rufani Jaji Salum Massati
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni