MAHAKAMA YA
TANZANIA
TANGAZO KWA UMMA
MAHAKAMA YA TANZANIA INAPENDA
KUWAJULISHA WANANCHI NA WADAU
1. HUDUMA YA MAHAKAMA INAYOTEMBEA ‘MOBILE COURT SERVICES’
2. KUSIKILIZA BAADHI YA MASHAURI KWA NJIA YA MTANDAO KWA KUTUMIA MAHAKAMA MTANDAO ‘VIRTUAL COURT’
3. ELIMU JUU YA HUDUMA NA TARATIBU MBALIMBALI ZA UFUNGUAJI WA MASHAURI YAKIWEMO MASHAURI YA MIRATHI.
4. KUELEZEA MFUMO WA KUSAJILI, KURATIBU NA KUSIMAMIA UENDESHAJI WA MASHAURI (JSDS)
5.KUTOA MAELEKEZO YA UPATIKANAJI WA MAAMUZI KWA NJIA YA MTANDAO
6. KUELEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA NGAZI MBALIMBALI ZA MAHAKAMA IKIWEMO DIVISHENI ZA MAHAKAMA KUU
7. KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHU MALALAMIKO YA WANANCHI
8. KUTOA FOMU ZA UDAHILI NA KUZIPOKEA AMBAPO HUDUMA HII ITATOLEWA NA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA)
9. MSAADA WA KISHERIA ‘TLS’
AIDHA; KATIKA MAONESHO HAYO MAHAKAMA YA TANZANIA IPO KATIKA BANDA MOJA PAMOJA NA BAADHI YA WADAU WAKE AMBAO NI CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA-LUSHOTO, (IJA), CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS), CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA) PAMOJA NA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI (EACJ), AMBAO WOTE WATATOA ELIMU KUHUSU MAENEO YAO.
HUDUMA TAJWA ZINATOLEWA NDANI YA BANDA LA MAHAKAMA, LILILOPO MKABALA NA BANDA LA JKT KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE ‘SABASABA’ DAR ES SALAAM.
HUDUMA HIZO ZITATOLEWA HADI JULAI 08, 2021.
EWE MWANANCHI, KARIBU UPATE ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.
WOTE MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA NA;
KITENGO
CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni