Na Francisca Swai, Musoma
Mahakimu
Wakazi Kanda ya Musoma wanolewa kikamilifu katika kikao kazi kilichoandaliwa na
Mhe. Jaji. Mfawidhi wa Kanda ya Musoma Mhe. Jaji, John Kahyoza ambapo, Mahakimu
hao walikumbushwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na taratibu mbalimbali katika
usikilizaji wa Mashauri mbalimbali.
Katika
kikao kazi hicho kilichofanyika hivi karibuni, Mahakimu hao walipewa jukumu la
kuandaa na kuwasilisha mada tofauti tofauti na kisha kufanyika majadiliano ya
pamoja.
Mada
zilizowasilishwa ni pamoja na Tabia na mwenendo wa Maadili kwa Maafisa wa
Mahakama, Hatua muhimu za kuzingatia katika uendeshaji wa Mashahuri ya Jinai
tangu kufunguliwa hadi kufikia hukumu, Ufunguaji wa kesi katika Mahakama za
Mwanzo.
Nyingine
ni hatua za utekelezaji wa hukumu katika Mahakama za Mwanzo, Jinsi ya
kushughulikia mapingamizi katika mashauri ya mirathi Mahakama za Mwanzo na
Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai katika Mahakama za Mwanzo.
Washiriki
wa kikao kazi hicho walimpongeza Mhe. Jaji. Kahyoza kwa kuandaa kikao hicho kwani
kimesaidia kuwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia katika utendaji kazi wa kila
siku na pia kimekuwa msaada kwa Mahakimu ambao ndio wameanza kazi.
Picha ya pamoja ya washiriki wote wa kikao kazi
cha Waheshimiwa Mahakimu Mahakama Kanda ya Musoma. Waliokaa katikati ni
Mhe, Jaji. John Kahyoza, Jaji Mfawidhi Mahakama Kanda ya Musoma, kulia
kwake ni Mhe, Jaji. Ephery Sedekia Kisanya, Jaji wa Mahakama Kuu Musoma.
Kushoto kwake ni Naibu Msajili Mhe. Mary Moyo na kushoto kwake ni Mhe.
Tumaini Marwa, Kaimu Hakimu Mkazi Mahakama ya Mkoa, na mwisho kushoto ni Bw.
Festo Chonya, Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma.
Mhe. Jaji. JohnKahyoza
akielezea jambo katika kikao kazi hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni