Alhamisi, 29 Julai 2021

TANZIA; MAHAKAMA YA TANZANIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTUMISHI WAKE


Marehemu Selemani Hussein Ngawanae enzi za uhai wake.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Selemani Hussein Ngawanae (Pichani) aliyekuwa Dereva wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora zinaeleza kuwa Marehemu Ngawanae amekutwa na umauti alfajiri ya kuamkia Julai 28,2021 katika Hospitali ya Rufaa Kitete Manispaa ya Tabora.

Taratibu zingine za mazishi zitatolewa hapo baadae, baada ya kukamilika kwa mipango ya kifamilia.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE, AMEN.


 

Maoni 1 :