Ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Haydom, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara uko mbioni kukamilika.
Hayo yamebainishwa na Uongozi wa Mahakama ya Mkoa wa
Manyara kufuatia ziara ya ki kukagua mradi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa jengo hilo
linatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 09, mwaka huu.
Katika kikao ‘site meeting’ kilichofanyika mara
baada ya ukaguzi ambacho kilihudhuriwa na Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Manyara Bwana
Jacob Swalle, Meneja wa TBA Mkoa wa Manyara
Bwana Wilson Tesha na Mwakilishi wa kamupuni ya ECO GREEN Construction Co
Ltd (ambaye ni Mkandarasi wa Jengo hilo) Bwana Noah Haki, ilibainika kuwa jengo
hilo limekamilika kwa kiasi cha asilimia 65.
Mradi wa Ujenzi wa jengo hilo ulianza tarehe 03/03/2021. Mahakama ya Mwanzo Haydom inatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakisafiri kwenda Dongobesh kwa ajili ya huduma za kimahakama ambapo kuna umbali wa Kilometa 45.
Meneja wa 'TBA' Mkoa wa Manyara, Bw.Wilson Tesha (wa pili kushoto) na Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Manyara, Bw. Jacob Swalle (wa kwanza kulia) wakiendelea na Ukaguzi wa Jengo hilo.
Muonekano wa Vyoo vya Wateja watakaokuwa wanafika Mahakamani.
(Picha na Christopher Msagati-Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni