TANZIA
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha
Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Serengeti-Mara, Mhe. Ismael Emmanuel Ngaile (pichani) kilichotokea siku ya
Jumatano Agosti 11, 2021 majira ya saa 3 usiku.
Kwa
mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Uongozi wa Mahakama Kuu, Kanda ya
Musoma marehemu Ngaile alikutwa na umauti katika hospitali ya Nyerere DHH
iliyoko wilayani Serengeti alipokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu
Ngaile aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania Juni 27, 2006, na alifanya kazi
katika vituo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Wilaya Kibondo..
Taratibu
za mazishi zinaendelea, aidha; taarifa za awali zinasema kuwa marehemu atapumzishwa
nyumbani kwake wilayani Kahama.
Mahakama ya
Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia
msiba huu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE
LIHIMIDIWE.
Pumzika kwa amani Mhe. Ngaile
JibuFuta