Alhamisi, 19 Agosti 2021

UJUMBE WA PROGRAMU YA BSAAT WAITEMBELEA MAHAKAMA

PROGRAMU YA KITAIFA YA KUZIJENGEA UWEZO TAASISI ZA UMMA ZINAZOHUSIKA NA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA - BSAAT

UJUMBE HUO KUTOKA UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA UMEITEMBELEA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI PAMOJA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM, leo Agosti 19, 2021.

UJUMBE HUO ULIFANYA MAZUNGUMZO YA KUTAMBUA MAENEO YA KUSHIRIKIANA NA MAHAKAMA.

Ujumbe wa Programu ya BSAAT wakiwa kwenye picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama ya Tanzania - Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul Kihwelo (wa pili kushoto) mara baada ya mazungumzo ya mashirikiano baina ya Taasisi hizo, wengine ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Elinaza Luvanda, (wa kwanza kushoto) na Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Emmaculate Banzi (wa kwanza kulia) na mwenye miwani mstari wa nyuma ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Bw. Elia Machumu.

Ujumbe wa Programu ya BSAAT wakiwa kwenye picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama ya Tanzania - Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul Kihwelo (wa kwanza kushoto) mara baada ya mazungumzo ya mashirikiano baina ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Taasisi hiyo, (kulia wa kwanza) ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mhe. Godfrey Isaya.


Mjumbe wa Programu ya BSAAT kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini akifafanua jambo wakati wa kikao hicho na  majadilianao ya namna ya mashirikiano na Viongozi waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Mjumbe wa Programu ya BSAAT kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini akielezea jambo wakati wa kikao hicho.


Picha na Innocent Kansha - Mahakama

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni