Uongozi wa
Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi
wake Bw. Jackson Itanisa Mrefu (pichani) aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi Mkuu, Mahakama ya Mwanzo Mwandiga- Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mahakama Kanda ya Kigoma, Marehemu Itanisa alifikwa na umauti usiku wa tarehe 28.09.2021 katika hospitali ya ‘Baptist’ Kigoma alipokuwa akipatiwa matibabu mara baada ya kuugua ghafla tangu tarehe 25/09/2021.
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuusafirisha mwili kwenda Wilaya ya Sengerema kata ya Kasenyi ambapo mazishi yatafanyika.
Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
BWANA AMETOA
NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni