Jumatano, 6 Oktoba 2021

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA TUNDURU AFARIKI DUNIA


 Marehemu Said Issa Omari enzi za uhai wake.

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania, unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtumishi wake, Mlinzi wa Mahakama ya Wilaya Tunduru, marehemu Said Issa Omari (pichani).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mahakama, Kanda ya Songea zinasema kuwa Marehemu Omari alikutwa na umauti alfajiri ya tarehe 05/10/2021 katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni