Mhe. Agnes Neema Mhina enzi za uhai wake.
TANZIA
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Mhe. Agnes Neema Mhina (katika picha juu) aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Hai-Moshi Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt, Mhe. Agnes amekutwa na umauti leo tarehe 06 Desemba, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mahakama Kuu-Masjala Kuu, mwili wa marehemu utaagwa kesho tarehe 07 Desemba, 2021 saa 06:00 mchana katika kanisa Katoliki la Muhimbili, mnamo tarehe 08 Desemba, 2021 mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea Lushoto kwa ajili ya kuaga ambapo baada ya hapo wataelekea Wilaya ya Muheza-Tanga katika kijiji cha Tonga kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika tarehe 09.12.2021.
Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni