Jumamosi, 29 Januari 2022

JAJI MRUMA : ONGOZENI UBUNIFU ILI MAONESHO YAVUTIE WATU WENGI

 

Na Magreth Kinabo

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Amir Mruma amewataka watumishi wa kanda hiyo kubuni mbinu zitakazoweza kuwavutia watu wengi kupata elimu ya sheria katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 29, Januari, wakati Jaji huyo wakati akifunga maadhimisho hayo ya kanda hiyo, yaliyoanza kuanzia tarehe 23 Januari kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu iliyopo Jijini Dar es Salaam.

‘‘Maadhimisho haya ni ya kitaaluma, hivyo inabidi tuongeze nguvu za ubunifu ili yaweze kwavutia watu wengi, kama iliyo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kwa jina la sabasaba, hivyo tubuni namna ya wadau wetu kuweza  kupata elimu ya sheria,’’ alisema Jaji Mruma.

Aliongeza kwamba ili kuongeza ushiriki wa wadau ipo haja ya kutoa cheti cha ushiriki.

Hata hivyo aliwashukuru wadau na watumishi wa Mahakama wa kanda hiyo kwa kushiriki katika maonesho hayo.

Kwa upande wake Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dares Salaam, Mhe. Victoria Nongwa alisema kupitia maadhimisho hayo, wameweza kufanya matembezi kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania hadi kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa elimu ya sheria kwenye maeneo mbalimbali, zikiwemo shule za sekondari zipatazo 18 na wodi za wakina mama katika hospitali tano na kutoa msaada kwa watoto yatima.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni