Alhamisi, 27 Januari 2022

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA

Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wanaendelea kutembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma yalioanza tarehe 23 Januari, 2022. Ikiwa ni siku ya tano ya Maonesho haya, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini naye amepata nafasi ya kutembelea maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja tajwa.

Mhe. Sagini ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa Maonesho mazuri yaliyopangiliwa vizuri huku akitoa rai kuitangaza zaidi wiki ya sheria ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na maonesho hayo.

Matukio katika Picha-Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonesho ya Wiki Ya Sheria Nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza jambo na Maafisa kutoka Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ambapo alipata nafasi ya kutembelea banda hilo leo tarehe 27 Januari, 2022. Aliyeshika Kipaza sauti 'mic' ni Bi. Dorothy Moses, Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akipata maelezo kutoka kwenye banda la Jeshi la Polisi wakati alipotembelea Mabanda ya Wiki ya Sheria katika Viwanja vya Nyerere 'Square' jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Uhamiaji kutoka kwa Afisa kutoka Ofisi hiyo.

Mkaguzi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Bi. Ndekela Mwakipesile (kulia) akitoa maelezo ya majukumu mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini wakati alipotembelea banda la Jeshi hilo linaloshiriki katika Maonesho ya Wiki ya Sheria Nchini yatakayohitimishwa tarehe 29 Januari, 2022 na kilele chake tarehe 01 Februari, 2022.

 Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Charles Magesa (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu Maonesho ya Wiki ya Sheria kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini aliyetembelea Maonesho hayo leo tarehe 27 Januari, 2022.

(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni