Na Tiganya Vincent – Mahakama, Dodoma
Jaji Mfawidhi Mahakama
Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu amewataka wajumbe wa Tume ya Utumishi
ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji kuhakikisha wanaisoma
na kuielewa sheria inayosimamia majukumu ya chombo hicho.
Mhe. Mdemu ametoa kauli
hiyo leo tarehe 3 Februari, 2022, Jijini Dodoma mara baada ya kuwaapisha
wajumbe wa Tume hiyo.
Alisema watumishi wa
Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji ni vema wakapewa elimu kuhusu
sheria na taratibu ili utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo yafanyike vizuri na
kuepeka kwenda nje kutafuta suluhu.
“Elimu hii ya majukumu ya
Tume ishiishie kwa viongozi na wakuu wa vyombo ambavyo viko ndani ya Tume ,
bali iende kwa watumishi ambao wanawajibika kwenye Tume, kwani wao ndio wanaojua
taratibu za nidhamu wanazotakiwa kuzingatia ili waweze kuendelea kutekeleza
majukumu yao kwa uadilifu,”alisisitiza.
Mwenyekiti wa Tume hiyo
ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni (Mb) amemwakikishia
Jaji Mfawidhi huyo kuwa wajumbe watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa
uadilifu na weledi wa juu kwa ajili ya maendeleo ya vyombo vinavyosimamiwa Tume
na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Hamad Masauni (Mb) akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa wa Tume ya Utumishi ya
Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji tarehe 3 Febuari,
2022 . Anayemwapisha ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma,
Mhe. Gerson Mdemu.
1. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni (Mb) akisaini kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji tarehe 3 Febuari , 2022.
1 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe Jumanne Sagini (Mb) akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa wa Tume ya Utumishi
ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji tarehe 3 Febuari
, 2022.
Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
John Masunga akila kiapo cha kuwa Mjumbe
wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na
Uhamiaji tarehe 3 Febuari , 2022.
1.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji John Masunga akipokea hati za
kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na
Uokoaji na Uhamiaji tarehe 3 Febuari , 2022.
1. Kamishna wa Polisi(CP) Awadhi Juma Haji akila
kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza,
Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji tarehe 3 Febuari , 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni