Jumanne, 22 Februari 2022

JAJI NDUNGURU AZINDUA KIKAO MAALUM CHA MASHAURI YA MAUAJI KATAVI

Mashahidi 86 kusikilizwa

     Na James Kapele,  Mahakama-Katavi

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Dunstan Ndunguru amefungua kikao cha kusikiliza mashauri ya mauaji kitakachohusisha jumla ya mashahidi 86 kwenye mashauri nane.

Kikao hicho kilichozinduliwa tarehe 21 Februari, 2022 kwa gwaride maalum, kitaketi katika jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi ambapo mashauri hayo yatasikilizwa na kutolewa uamuzi.

Aidha, kikao hicho kitahusisha pia mashauri mengine tisa (9) ambayo washitakiwa watasomewa mashtaka yao na hoja za awali. Sambamba na mashauri hayo, Mahakama imeweka kwenye orodha jumla ya mashauri matano (5) ya mauaji yatakayosikilizwa iwapo wasaa wa kuyasikiliza utapatikana.

Kikao hiki kinatarajiwa kukamilika tarehe 22 Machi, 2022 ambapo pamoja na mambo mengine kinalenga kupunguza mashauri ya muda mrefu pamoja na msongamano wa mahabusu katika gereza lililopo Mpanda mjini. 

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Dunstan Ndunguru akikagua gwaride, shughuli hiyo ilifanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi. 

Baadhi ya askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia cha mkoani Katavi walioshiriki katika gwaride la ufunguzi wa kikao hicho.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Dunstan Ndunguru   akipokea salamu kutoka kwa kiongozi wa gwaride.
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni