TANZIA
Marehemu Alex Ramadhani Ulimwengu enzi za uhai wake.
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania, unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mtumishi wake Bw. Alex Ramadhani Ulimwengu aliyekuwa Mlinzi Mwandamizi katika Mahakama ya mwanzo Ilagala wilayani Uvinza
Marehemu Ulimwengu alifikwa na umauti mnamo tarehe 19 Februari, 2022 majira ya saa 10:30 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania kwa nafasi ya Mlinzi tangu tarehe 15/12/1999
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuusafirisha mwili kutoka Dar es Salaam kwenda Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo mazishi yatafanyika kesho tarehe 22 Februari, 2022 katika makaburi ya eneo la Masanga.
Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni