Ijumaa, 25 Februari 2022

TANZIA, MTUMISHI MAHAKAMA YA MWANZO MBAGALA DAR ES SALAAM AFARIKI DUNIA

Marehemu Zubeda Miraji Omary enzi za uhai wake.

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania, unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bibi. Zubeda Miraji Omary (katika picha) aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi, Mahakama ya Mwanzo Mbagala-Dar es Salaam.

Bibi Zubeda alikutwa na umauti usiku wa kuamkia leo tarehe 25 Februari, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo-Mbagala, Mhe. Florence Madelemo amesema mazishi yanafanyika leo saa 10:00 jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Mapipa-Dar es Salaam.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni