Jumatatu, 7 Machi 2022

JAJI MWASEBA AAGWA NA WATUMISHI KITUO JUMUISHI - TEMEKE

Na Amina  Said-  Mahakama  

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha masuala kifamilia (IJC) Mhe. Nyigulila Mwaseba ameagwa na watumishi wa kituo hicho, kilichopo wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Hafla hiyo fupi ya kumuaga Jaji Mwaseba ilifanyika kituoni hapo, baada kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, pamoja na kumkaribisha Jaji mpya wa kituo hicho, Mhe. Modesta Opiyo.

Akizungumza katika ghafla hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Temeke Mhe. Ilvin Mugeta alimuelezea Jaji Mwaseba kwamba watumishi wa hao wanashukuru katika kipindi chote walipokuwa naye na watahakikisha wanayaenzi yale yote aliyowaachia na kuwafundisha.

Jaji Mwaseba baada ya kupata fursa ya kuwaaga watumishi hao alisema, “nimefurahi kufanyiwa tukio hili la kihistoria, kwangu ni jambo kubwa. Nafahamu nawaacha katika kituo hiki, ila kwakuwa baadhi yenu tuliwahi kufanya kazi maeneo mengine kabla ya hapa, nina imani hata hapo baadae tunaweza kukutana tena,”alisema.

Kwa upande wake Mhe. Jaji Opiyo ambaye amehamia katika kituo hicho hivi karibuni, amewaahidi watumishi kufanya nao kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu katika kutekeleza azma ya utoaji wa haki kwa wakati.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Temeke, Mhe. Mary Moyo (aliyesimama) akizungumza katika hafla hiyo. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Temeke, Mhe. Ilvin Mugeta akifuatiwa na Mhe. Jaji Nyigulila Mwaseba kwa upande wa kulia. Kushoto ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Anna Mpessa akifuatiwa na Mhe. Jaji Modesta Opiyo ambaye amehamia kituo Jumuishi Temeke hivi karibuni.

Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Temeke, Mhe. Ilvin Mugeta, akimlisha keki Mhe. Nyigulila Mwaseba ikiwa ni ishara ya kumuaga na kumtakia mema katika kituo chache kipya kanda ya Arusha.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Temeke, Mhe. Mary Moyo (kushoto) akimkabidhi zawadi Mhe. Jaji Modesta Opiyo (kulia), ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha masuala ya kifamilia- Temeke. Katikati ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Anna Mpessa. 

               Baadhi ya watumishi walioshiriki katika hafla hiyo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni