Alhamisi, 17 Machi 2022

KAMATI YA KATIBA NA SHERIA YAENDELEA NA UKAGUZI WA MIRADI YA MAHAKAMA

-Yafanya ukaguzi katika Mradi wa Ujenzi wa Mahakama wa Wilaya Mwanga

-Mradi wa ukarabati wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi

Ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeendelea na ziara yake ya kukagua Miradi mbalimbali ya Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu ya Majengo ya Mahakama ambapo leo tarehe 17 Machi, 2022 imetembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Mwanga na vilevile imekagua Mradi wa Ukarabati wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi-Kilimanjaro.

MATUKIO KATIKA PICHA:ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA NDANI YA MAHAKAMA

Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Mwanga lililokaguliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, jengo hili lipo katika hatua za mwisho na linatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Aprili mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha kitu Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria walipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Kamati hiyo ilianza ziara yake tarehe 15 Machi, 2022 imekwishatembelea pia Mradi wa Jengo la Kuhifadhi Kumbukumbu za Mahakama-Mahakama Kuu Tanga, Mradi wa Bweni la Wavulana katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Same na itahitimisha ziara yake kwa kukagua Mradi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Arusha.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel  akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria sehemu ya ndani ya jengo la Mahakama ya Wilaya Mwanga lililopo katika hatua za mwisho za ujenzi wake.

Kikao mara baada ya ukaguzi - Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

Picha ya pamoja:Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Watumishi wa Mahakama pamoja na Watumishi wa Wilaya ya Mwanga. Waliosimama mbele (katikati) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Emmanuel Mwakasaka, wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geofrey Pinda, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Kazungu Khatibu, wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Anania Thadayo, wa nne kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, wa nne kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Abdallah Mwaipaya.

Ukaguzi wa Mradi wa Ukarabati wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.


Muonekano wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi linalofanyiwa ukarabati.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Mwanga&Moshi)

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni