Na Innocent Kansha – Mahakama, Songea
Mahakama
za Wilaya Mbinga na Nyasa zimejivunia mafanikio lukuki kutokana na utendaji kazi
wa watumishi wazalendo wenye ari ya kujituma na kujali muda wa kufanya kazi kwa
bidii.
Wakisoma
ripoti ya utendaji kazi wa Mahakama hizo kwa nyakati tofauti mbele ya Jaji Mkuu
wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakati wa ziara yake ya kikazi ya Mahakama,
Kanda ya Songea leo tarehe 28 Februari, 2022, Mahakimu Wafawidhi Mhe. Ally
Mkama na Mhe. Osmund Ngatunga wameeleza mfanikio hayo, hasa katika usikilizaji
wa mashauri.
Mhe.
Mkama kutoka Mahakama ya Wilaya ya Mbinga alisema katika kipindi cha robo ya
kwanza ya mwaka 2022, Mahakama imefanya kikao cha kusukuma mashauri “Case flow
Management” na kutembelea gereza la Mahabusu Mbiga Mjini na kufanya ukaguzi wa
Mahakama za Mwanzo.
“Mahakama
ya Wilaya kupitia vikao vyake vya kusukuma mashauri tumefanikiwa kuendesha
vikao vya kimkakati vya kumaliza mashauri ya muda mrefu “Back Log” na kupanga
mpango wa kutozalisha mashauri mengine ya muda mrefu yaani “Back Stoping”,
alibainisha Mfawidhi huyo.
Mhe.
Mkama aliongeza kuwa kwa upande wa mashauri ambayo hawana mamlaka nayo, Mahakama
na wadau wa haki jinai wamejiwekea mkakati wa usikilizaji wa mashauri hayo na umalizaji
wa upelelezi wake mfano: mashauri ya mauaji na uhujumu uchumi kufanyika ndani ya
miezi sita (6) tu ili kuruhusu mamlaka nyingine kukamilisha upelelezi kwa hatua
zilizobaki.
Hakimu
Mfawidhi huyo alisema, Mahakama ya Wilaya Mbinga imefanikiwa kufanya vikao
Viwili (2) vya Kamati ya maadili ya Maafisa wa Mahakama chini ya Mwenyekiti wa
kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo ikiwa ni kutimiza majukumu yake ya
kusimamia nidhamu kwa Mahakamu.
Mafanikio
mengine aliyoyataja Mhe. Mkama ni pamoja na kupunguza madeni ya ofisi kutoka
kwa wazabuni na watumishi wanaodai stahiki mbalimbali, kwani ofisi inahakikisha
kuwa inapunguza matumizi yasiyo ya lazima yanayoweza kusababisha madeni.
Ununuzi
wa vitendea kazi vya Ofisi kama vile samani, vifaa vya TEHAMA, ukarabati wa
baadhi ya majengo na kuendelea kwa ujenzi wa jengo la hadhi ya karne ya 21la
Mahakama ya Mwanzo Matiri.
Mhe.
Mkama aliongeza kuwa Mahakama ya Wilaya Mbinga imefanikiwa kusajili mashauri
yote kwa njia ya mtandao “E- Failing” katika kipindi cha mwaka 2021 hadi
kufikia mwezi Februari 2022.
“Katika
kuhakikisha utekeleza wa mpango wa Mahakama kwa Mahakama zote zina viwanja
vyenye hati miliki, hadi sasa Mahakama ya Wilaya Mbinga imeshapata hati sita
(6) za Mahakama za Mwanzo Ndengu, Mkumbi, Matiri, Litembo na Mahakama ya Wilaya
Mbinga wakati Mahakama za Mwanzo Ruanda na Kigonsera zipo katika hatua za
mwisho kukamilisha upatikanaji wa hati hizo”, alisema Mhe. Mkama
“Tumefanikiwa
kusimamia nidhamu kwa watumishi kwani hadi sasa hakuna mtumishi yeyote
aliyefikishwa mahakamani au kwenye Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa makossa ya
maadili”, alisisitiza Hakimu Mfawidhi huyo
Kwa
upande wake, Mhe. Ngatunga kutoka Mahakama ya Nyasa alisema usajili wa mashauri
kwa njia ya mtandao kwa mwaka 2021 ulikuwa ni asilimia 80 ya mashauri yote yaliyosajiliwa
kwa njia hiyo na kwa mwaka 2022 ni asilimia 100 mashauri yamesajiliwa kwa njia
ya mtandao.
“Tumefanikiwa
kupata viwanja vine (4) kwa ajili ya kujenga majengo ya Mahakama, kati ya hivyo
viwanja kipo ambacho kimetengwa kwa ajili ya kujenga jengo la Mahakama ya
Wilaya Nyasa chenye ukubwa wa mita za mraba 16,920, kipo katika hali nzuri na
kinafaa kutumika katika ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya”, alisema Mhe.
Ngatunga.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (mwenye tai nyekundu kulia) akionyeshwa eneo la kiwanja litakapo jengwa jengo la Mahakama ya Wilaya Nyasa, aliyenyoosha mkono wa pili kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama Wilaya Nyasa Mhe. Osmund Ngatunga akiendelea na zoezi wakati wa ziara yake ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (mwenye tai nyekundu wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Nyasa, wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Laban Thomas, wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Songea, Mhe. Sekela Moshi na wa kwanza kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Martin Chuma wakati wa ziara ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akimkabidhi Kalenda ya Mahakama ya mwaka 2022 Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Aziza Mangosongo Ofisini kwake.
Picha na Innocent kansha na Faustine Kapama - Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni