Ijumaa, 25 Machi 2022

MSAJILI MKUU AHIMIZA BUSARA, LUGHA NZURI KITUO HUDUMA KWA MTEJA

 Na Faustine Kapama – Mahakama.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, leo tarehe 24 Machi, 2022 amekutana na maafisa wanaofanyakazi kwenye kituo cha huduma kwa mteja (Call Center) na kuwaelekeza namna bora ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi.

Katika semina hiyo fupi iliyohudhuliwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za Kimahakama, Malalamiko na Maadili, Mhe. Annah Magutu, Msajili Mkuu huyo pia amehimiza maafisa hao kufanyakazi kwa weledi na uadilifu wa kiwango cha juu.

Kadhalika, aliwajulisha kuwa kazi wanayofanya ni ya usiri. Hivyo wanapaswa kuifanya kwa busara, hekima, uvumilivu, kujiamini na kwa lugha nzuri kwa walamikaji. 

Aidha, amewawahimiza kuhakikisha malalamiko yanashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo na kuwaelimisha wananchi uwepo wa Kamati za Maadili za Mikoa na Wilaya.

Baada ya semina hiyo, Mhe. Chuma aliwakabidhi maafisa hao miongozo mbalimbali inayoelekeza namna ya kushughulikia malalamiko na kuwahudumia wananchi.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma akiongea na maafisa wanaofanya kazi kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja alipokutana nao leo tarehe 24 Machi, 2022 kwa semina fupi.

Sehemu ya maafisa wanaofanyakazi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja wakiwa kwenye semina fupi na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma.

 

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma (kulia) akikabidhi mwongozo wa kazi kwa maafisa wa Kituo hicho, Evatha Mboya (kushoto) na Dominician Mlashani (anayetazama kamera). Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za Kimahakama, Malalamiko na Maadili, Mhe. Annah Magutu(wa pili kulia).
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Kituo hicho.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni